VIDONDA VYA TUMBO

VIDONDA VYA TUMBO - Tanzania
VIDONDA VYA TUMBO - Tanzania
  • VIDONDA VYA TUMBO - Tanzania
  • VIDONDA VYA TUMBO - Tanzania
Description :

FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO

Ni vidonda vilivyo wazi ambavyo hutokea katika kuta za tumbo,sehemu ya juu ya utumbo mdogo au kwenye kuta za koromeo kutokana na bacteria waitwao H.pylori na asid inayozalishwa kwenye kuta za tumbo.

Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito. nk

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO

Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;

Ø Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
Ø Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin(bayer), (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
Ø Msongo mawazo (stress)
Ø Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
Ø Kunywa pombe na vinywaji vikali kupitiliza.
Ø Uvutaji wa sigara.
Ø Kuto kula mlo kwa mpangilio maalumu
Ø Kansa ya tumbo


DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na kuendelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vina dalili kama;

Ø Kupata maumivu ya tumbo ya kuwaka moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
Ø Kupatwa na kiungulia(heartburn) karibu na chembe ya moyo
Ø Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
Ø Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
Ø Kupata haja kubwa ya rangi ya kahawia au nyeusi cheenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
Ø Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
Ø Kushindwa kupumua vizuri.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data