Usisumbuke Tena Na Hormone Imbalance

Usisumbuke Tena Na Hormone Imbalance - Tanzania
  • Usisumbuke Tena Na Hormone Imbalance - Tanzania
Description :

Matatizo ya homoni ndiyo yenye mchango mkubwa zaidi kwenye kumfanya mwanamke ashindwe kuzalisha mayai. Uzalishwaji wa mayai hutegemea mchanganyiko wa homoni utakaofanya kazi kwa kuhusiana bila kuvurugwa katika utendaji wake wa kazi.

Kuna matatizo ya aina tatu yanayoweza kuvuruga mpangilio huo.

1. Kuzalisha Mayai Yasiyokomaa: Hiki ni kipindi kati ya mwanzo wa hedhi hadi kuachiwa kwa yai (ovulation.) Ishara kutoka kwenye ubongo huagiza ovari kuandaa yai litakaloachiwa.

Ndani ya kipindi hiki, tezi ya pitutary (eneo dogo chini ya ubongo linalotengeneza homoni) hutoa homoni iitwayo follicle stimulating hormone (FSH). FSH huziagiza ovari kuandaa yai kwa ajili ya kuachiwa. Inapofika nusu ya kipindi hiki, follicle (kifuko cha majimaji chenye yai) moja kutoka moja ya ovari huwa ni kubwa kuliko follicle nyingine zote (kama sentimeta 1). Follicle hii huwa ndiyo inayoandaliwa kutolewa wakati wa ovulation. Follicle hii hutoa homoni ya estrogen wakati ikikua, na hufikia kilele mara tu kabla ya yai kutolewa (ovulation). Kwa wanawake wengi kipindi cha follicular hudumu siku 10-22, lakini muda huweza kubadilika kutoka mzunguko mmoja hadi mwingine.

Kuanzia siku yai linapoachiwa hadi mwanzo wa hedhi ya pili. Mfuko uliokuwa na yai unazalisha estrogen na progesterone.

Baada ya yai kuachiwa, follicle iliyokuwa na yai hugeuka kuwa corpus luteum na huanza kuzalisha progesterone pamoja na estrogen. Progesterone hufikia kiwango cha juu katikati ya kipindi hiki. Mabadiliko ya homoni katika kipindi hiki ndiyo yanayosababisha dalili mbambali ambazo wanawake huzipata kabla ya hedhi; kama, mabadiliko ya kitabia, kuumwa kichwa, chunusi, na maumivu kwenye matiti.

Kama yai litapevushwa, progesterone kutoka kwenye corpus luteum itasaidia kwenye hatua za mwanzo za ujauzito. Kama yai halitarutubishwa, corpus luteum itaanza kujivunjavunja siku 9 hadi 11 baada ya yai kuachiwa. Hii itasababisha viwango vya estrogen na progesterone kushuka, na kusabibisha hedhi.

Wakati homoni ya estrogen ni muhimu, progesterone ni ya muhimu zaidi katika kipindi hiki.

2. Matatizo Ya Hypothalamus: Hypothalamus ni sehemu ya ubongo inayohusika na kutoa ishara kwa tezi ya pituitary (pituitary gland) ambayo nayo huamsha homoni za ovari zinazoruhusu yai kukomaa. Hypothalamus isipofanya kazi yake, mayai hushindwa kufika ukomavu. Asilimia 20 ya dosari za ukomavu wa mayai husababishwa na matatizo ya hypothalamus.

3. Matatizo Ya Pituitary Gland: Tumeona hapo juu kuwa tezi ya pituitary inahusika katika kukomaza mayai. Endapo pituitary itatoa homoni kwa kiwango kidogo au kikubwa kupita kiasi, ovari zitashindwa kuzalisha na kutoa mayai ipaswavyo. Hali hii hutokea pale tezi hii inapoharibiwa kwa ajali, kunapotokea uvimbe ndani yake au kunapokosekana ulingano wa kikemikali ndani ya tezi hiyo.

Kupata maelezo ya kina au tiba, tutembelee ofisini, tupo mtaa wa Lindi, ndani ya majengo ya Machinga Complex, eneo la Karume.

Kwa walio nje ya Dar es Salaam, huduma ya kutuma mzigo kwa bus inatolewa.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • Never send money to "book" an item, avoid paying before seeing the it.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matching the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data