UNENE/KITAMBI

UNENE/KITAMBI - Tanzania
  • UNENE/KITAMBI - Tanzania
Description :

Madhara yake

Ugonjwa wa kisukari; hii ni ugonjwa ambao mwili hushindwa kupambana na wingi wa sukari uliopo ndani ya mwili wa binadamu kutoka kwenye chakula anachokula kila siku na hii huweza kusababishwa kutotengenezwa kabisa kwa homoni ya insulin[diabetes type one] au homoni ya insulin kushindwa kuingia ndani ya cell nene[fat cell] ambazo huwepo mtu akiwa mnene sana.

Ugonjwa wa moyo: mafuta mengi ndani ya mwili wa binadamu hujaa kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kupita kirahisi hivyo moyo hutanuka na kuongezeka ukubwa ili utengeneze presha kubwa ya kusukuma damu ndani ya mishipa hiyo na dakika za mwisho moyo hushindwa kabisa kufanya kazi.

Vifo vya ghafla sana: ukichunguza watu wengi ambao wamekufa ghafla ni wenye uzito uliopitiliza na watu hawa hufa usingizini na kukutwa marehemu asubuhi, hii ni kwasababu unene husababisha hali Fulani inaitwa sleep apnoea ambayo muhusika husimama kupumua kwa muda wakati amelala afu anendelea, wakati mwingine kusimama kwa kupumua kunasababisha kifo kabisa

kansa za aina mbalimbali; unene hufanya mwili kushindwa kupambana na seli zinazosababisha kansa hivyo mtu hua kwenye hatari ya kupata kansa ya figo, kansa ya kizazi, kansa ya utumbo mkubwa, kansa ya maini, kansa ya tezi dume, kansa ya kongosho, kansa ya koo, kansa ya matiti, kansa ya mlango wa uzazi na nyingine nyingi.

Kuishiwa nguvu za kiume

Ugumba kwa wanawake; unene husababisha homoni za wanawake kutokua katika mfumo mzuri[unbalanced] na pia wanawake hawa hupata sana kansa za mifuko ya uzazi yaani fibroids hali hii huweza kusababisha kutozaa kabisa.

Magonjwa ya jointi za miguu[osteoarthritis}; mwili hubeba uzito kulingana na urefu wa mtu husika, mtu akiwa mnene sana jointi za mwili hasa za miguuni[knee joints] huanza kuasagana na kusababisha maumivu makali mno na mtu hushindwa kutembea kabisa..

Presha ya damu; kama nilivyozungumzia kwenye tatizo la moyo linavyoanza, pia kitu kilekile hutokea kwenye mishipa ya damu mafuta yanapokua mengi.... yaani moyo hutumia nguvu nyingi kusukuma damu ili ifikie viungo vingine na hapo ndipo presha ya damu inapoanza.

Kiharusi[stroke]; hili ni tatizo linalotokea pale ambapo damu inaingia kwa presha kubwa kichwani na kupasua mishipa ya ubongo au mishipa ya ubongo inapoziba na mafuta..hii husababisha upande mmoja wa mwili wa binadamu kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi .

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data