Unashindwa Kumpa Mimba Mkeo?

Unashindwa Kumpa Mimba Mkeo? - Tanzania
  • Unashindwa Kumpa Mimba Mkeo? - Tanzania
Description :

Iweje mwanamme wa umri wa kuzaa ashindwe kumpa mimba mkewe?

Inapotokea kuwa mme na mke wanahangaika kupata mtoto, wote wawili wanaweza kuwa ndiyo sababu ya tatizo. Wanaume wanachangia kwa kiwango cha theluthi moja na wanawake pia wanachangia kwa theluthi nyingine moja. Theluthi inayobakia ni matatizo yanayowahusu wote wawili. Kuna mambo mengi ya kuyachunguza, lakini tatizo kuu huwa ni katika mbegu zake mwanamme. Katika somo letu la leo tutajadili kwa kina mambo ambayo yanaweza kusababisha mbegu za mwanamme zisiwe na uwezo wa kumpa mimba mwanamke.Upungufu wa Mbegu Za Kiume


Upungufu wa mbegu za kiume kitaalamu huitwa oligospermia. Hili ni neno linalotumika kuelezea hali ambapo idadi ya mbegu za mwanamme ni ndogo, pungufu ya mbegu milioni 15 katika mililita moja. Kama hakuna mbegu kabisa, hali hiyo huitwa azoospermia. Unapohitaji kupata mtoto, idadi ya mbegu unayotoa wakati wa tendo la ndoa ni muhimu. Idadi ya kawaida ya mbegu ni kati ya milioni 15 hadi milioni 200 kwa mililita moja.

Ni vigumu kidogo kulielezea tatizo la upungufu wa mbegu za kiume. Kuna vipimo vingi vya kuvichukua wakati wa kufanya semen analysis. Kwanza, kama tulivyosema hapo awali, utachunguzwa uwingi wa mbegu katika ujazo wa mililita moja. Kisha daktari atataka kujua ni mililita ngapi zinatolewa. Kwa mfano, mtu mwenye mbegu milioni 40 katika mililita na anakojoa mililita moja hawezi kuwa mzuri zaidi ya yule mwenye mbegu milioni 18 kwa mililita na kutoa mililita 4 za ujazo anapokojoa. Tunapenda kuona mbegu angalau milioni 20 kwa mililita na kiasi cha mililita 2 hadi 5 za ujazo zikitolewa kwa mara moja. Ujazo wa kawaida ni mililita 2.5, ambao ni sawa na nusu kijiko cha chai.

Kipimo kingine ni kuchunguza ni asilimia ngapi ya mbegu ambazo zina uwezo wa kutembea, sperm motility, ambapo tunasema asilimia 50 ya mbegu kuwa na uwezo wa kutembea kuelekea kwenye nyumba ya uzazi ndicho kiwango cha chini kinachotakiwa.

Ukubwa na maumbo ya mbegu ni kigezo kingine kwa mbegu kuwa na uwezo wa kulirutubisha yai. Uchuguzi unafanyika kuona kuwa ni asilimia ngapi ya mbegu zenye ukubwa na maumbo yaliyokamilika – sperm morphology. Mbegu safi inatakiwa kuwa na asilimia angalau 30 ya mbegu zenye ukubwa na maumbo kamilifu.

Kiwango cha pH cha shahawa ni muhimu vile vile na kiwango kizuri ni cha kati ya pH 7.1 na 8.0. Kiwango kidogo cha pH kinamaanisha mbegu ni za utindikali zaidi na kiwango kikubwa maana yake mbegu ni alkaline. Kiwango cha pH kinaweza kuathiri afya ya mbegu zako na jinsi zitakavyosafiri.

Mbegu zinapomwagwa huwa nzito. Mbegu hizi zinafaa kuchukua dakika kama 20 kabla ya kuwa nyepesi. Kama mbegu zako zinachukua muda mrefu zaidi au zinabaki nzito moja kwa moja, maana yake kuna tatizo.

Unapotazama uwezo wa mbegu kulirutubisha yai, lazima kuchunguza haya yote. Upungufu kidogo katika idadi ya mbegu, kwa mfano, unaweza kusaidiwa na mbegu kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutembea au mbegu kuwa na ujazo mkubwa sana.

Kwa maelezo zaidi, tembelea ofisi zetu zilizopo mtaa wa Lindi, ndani ya majengo ya Machinga Complex, eneo la Karume (DSM).

Huduma ya kuwatumia wateja wa mikoani kwa bus inatolewa.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • Never send money to "book" an item, avoid paying before seeing the it.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matching the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data