Ujue ugonjwa wa kisukari na Tiba

Ujue ugonjwa wa kisukari na Tiba - Tanzania
Ujue ugonjwa wa kisukari na Tiba - Tanzania
  • Ujue ugonjwa wa kisukari na Tiba - Tanzania
  • Ujue ugonjwa wa kisukari na Tiba - Tanzania
Description :

UJUE UGONJWA WA KISUKARI (Diabetes)
Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.
Ugonjwa wa Kisukari hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo (Homoni) aina ya insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kwa sukari (Hyperglycemia) au kushuka kwa kiwango cha sukari (Hypoglycemia). Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili

NI NANI ANAWEZA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI?
Watu walio katika makundi yafuatayo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kisukari:
 Wenye uzito uliozi
 Wenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari katika familia zao,
 Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,
 Watu wasiojishughirisha au wasiofanya mazoezi,
 Wenye shinikizo la damu,
 Wenye msongo wa mawazo na
 Wenye matumizi makubwa ya pombe na sigara
 Watu hawa wanashauriwa kupima sukari yao kila mwaka wakiwa na umri wa miaka 45 na kuendelea.
Kuna hatari kubwa ya kuugua ugonjwa

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
 Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati
 Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani
 Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
 Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
 Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
 Wanawake kuwashwa ukeni.
 Kutoona vizuri.
 Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
 Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole
 Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
 Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.
 Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
 Majipu mwilini.
Wenye dalili hizi wanashauriwa kupima sukari ili kubaini kama wana kisukari.
Watu wenye kisukari wanapaswa kubadili jinsi wanavyokula na kuishi.Ufuatao ni ushauri wa kuwasaidia

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data