Ujue ugonjwa wa bawasili na tiba yake

Ujue ugonjwa wa bawasili na tiba yake - Tanzania
  • Ujue ugonjwa wa bawasili na tiba yake - Tanzania
Description :

BAWASIRI ni ugonjwa unaojitokeza katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa Kiingereza ugonjwa huu huitwa Haemorrhoids au piles.

Bawasiri inaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini lakini unaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji au kwa kutumia dawa mbadala kwa kipindi cha kuanzia wiki sita na kuendelea, inategemea imejijenga kiasi gani.

Bawasiri husababishwa na nini?

Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kukufanya ukapata ugonjwa huu:

Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
Ujauzito; wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa.
Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
Uzee; kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu.
Sababu za kurithi; baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni kwa asilimia ndogo.
Kuharisha kwa muda mrefu.
Kutumia vyoo vya kukaa.
Kunyanyua vyuma vizito.
Mfadhaiko
Uzito na unene kupita kiasi.
Dalili zake

Ili kujua kama una ugonjwa huu ni lazima utasikia maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kinyesi kunuka damu wakati wa kujisaidia.

Dalili nyingine ni muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa, uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa na haja kubwa inaweza kutoka bila taarifa muda wowote.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data