Ufahamu ugonjwa wa kisukari na Namna rishe inavyoweza kukuokoa na janga hili

Ufahamu ugonjwa wa kisukari na Namna rishe inavyoweza kukuokoa na janga hili - Tanzania
  • Ufahamu ugonjwa wa kisukari na Namna rishe inavyoweza kukuokoa na janga hili - Tanzania
Description :

JE WAJUA KWAMBA KISUKARI HUSABABISHA KUKOJOA MARA KWA MARA NA KIU CHA MARA KWA MARA..!!?
Maelezo ya jumla
Kisukari (diabetes) ni ugonjwa unaoleta matatizo ya kimetaboliki ambayo husababisha kuwepo kwa viwango vya juu vya sukari katika damu kwa muda mrefu. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kukojoa mara kwa mara, kuwa na kiu sana, na kuhisi njaa sana.

Bila kutibiwa, ugonjwa wa kisukari unaweza kusababisha matatizo mengi. Matatizo haya yanaweza kuwa matatizo ya muda mfupi au matatizo makubwa ya muda mrefu ambayo ni pamoja na ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa figo, vidonda vya miguu, na uharibifu wa macho.

Kisukari husababishwa na kongosho kushindwa kuzalisha insulini ya kutosha ili kuingiza sukari kwenye seli za mwili na kwa sababu hii sukari hubakia kwenye damu na kuleta madhara makubwa. Seli za mwili zinaposhindwa kuitikia msisimo unaotolewa na insulini husababisha kisukari pia, hili husababishwa na usugu wa seli kwa insulini.

Kuna aina 3 kuu za ugonjwa wa kisukari:

Kisukari aina ya 1 ,husababishwa na kongosho kushindwa kuzalisha insulini ya kutosha kutokana na kupungua kwa seli za beta ambazo huzalisha insulini mwilini. Sababu ya kupungua kwa seli hizi haifahamiki vyema.

Kisukari aina ya 2, humpata mtu mwenye seli za mwili zenye usugu kwa insulini, hali hii husababisha seli za mwili kutoitikia vyema msisimuo unaotolewa na homoni ya insulini. Sababu kuu ya kupata aina hii ya kisukari ni unene wa mwili uliopitiliza na mazoezi yasiyotosha.

Kisukari cha Ujauzito, aina hii ya kisukari huwapata wanawake wajawazito na baada ya kujifungua hupona kabisa,na mara nyingi hawana historia ya kuwa na ugonjwa wa kisukari hapo awali.

Kinga na matibabu ya kisukari huhusisha kudumisha mlo ulio bora na mazoezi ya mwili ya mara kwa mara kudumisha uzito wa mwili unaofaa.

Kisukari aina ya 1 ni lazima itibiwe kwa sindano za insulini. kisukari aina ya 2 inaweza kutibiwa kwa dawa pekee au kwa dawa na insulini. Kisukari cha ujauzito kwa kawaida hupona baada ya mtoto kuzaliwa.

Kufikia mwaka wa 2015, watu milioni 415 ulimwenguni kote walidhaniwa kuwa na ugonjwa wa kisukari, kati ya wagonjwa wote 90% walikuwa na kisukari aina ya 2, idadi hiyo inawakilisha 8.3% ya idadi ya watu wazima wote duniani. [1]

Kufikia mwaka wa 2014, mwenendo ulipendekeza kuwa kiwango hicho kitaendelea kuongezeka. Ugonjwa wa kisukari unaongeza mara mbili hatari ya mtu kufa mapema. Kuanzia mwaka 2012 -2015, kumetokea vifo kati ya milioni 1.5 -5.0 kila mwaka kwa sababu ya ugonjwa wa kisukari. na gharama za kiuchumi za kisukari duniani kote mwaka 2014, ilikadiriwa kuwa bilioni 612 US$.[2]

Ishara na dalili za kisukari
Dalili za mgonjwa wa kisukari asiyekuwa kwenye tiba ni pamoja na: kupoteza uzito haraka, kukojoa sana,kuwa na kiu sana, na kuwa na hamu ya kula sana. Dalili za kisukari zinaweza kujitokeza kwa haraka sana (wiki au miezi) kwa kisukari aina ya 1,lakini kwa Kisukari aina ya 2 dalili hujitokeza taratibu na polepole, wakati mwingine zaweza kuwepo kidogo sana au zisiwepo kabisa.

Kuna dalili nyingine na ishara zinazoweza kuashiria mwanzo wa ugonjwa wa kisukari ingawa si maalum sana kwa ugonjwa huu, mgonjwa anaweza kuona maluweluwe,kichwa kuuma, uchovu, vidonda hupona polepole, na kuwashwa ngozi. Kiwango cha sukari katika damu kikiwa juu kwa muda mrefu husababisha lenzi ya jicho kuharibika na kusababisha matatizo ya macho.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu kwa ajili ya elimu zaidi na tiba pia kama utahitaji kujiunga kwenye group letu la afya

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • Never send money to "book" an item, avoid paying before seeing the it.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matching the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data