UCHAFU UNAO ITAJIKA UKENI NA USIO ITAJIKA AINA ZAKE

UCHAFU UNAO ITAJIKA UKENI NA USIO ITAJIKA AINA ZAKE - Tanzania
  • UCHAFU UNAO ITAJIKA UKENI NA USIO ITAJIKA AINA ZAKE - Tanzania
Description :

Kutokwa na uchafu ukeni ni jambo la kawaida kabisa kwa mwanamke. Hata hivo kuna aina zingine za uteute ambazo zaweza kuashiria kuna maambukizi.

Uchafu usiyo wa kawaida unaweza kuwa na rangi ya kijani, njano na wenye harufu mbaya. Maambukizi yanayowapata sana wanawake ni ya baketria ya ya fangasi na kupelekea kutokwa na uchafu usio wa kawaida unaoambatana na harufu mbaya.

Aina za Uchafu Ukeni
Kuna aina nyingi za uchafu ukeni. Aina zifuatazo zimegawanywa kwa kulingana na rangi na kiwango cha utokaji wake. Utaona kwamba aina zingine za uchafu ni salama na uchafu mwingine siyo salama, unaashiria kuwepo kwa ugonjwa

Uchafu Mweupe Ukeni
Kutokwa na uchafu mweupe hasa mwanzoni mwa hedhi au mwishoni mwa hedhi ni jambo la kawaida. Hata hivo kama uchafu huu unaambatana na muwasho na ni mzito sana kama maziwa ujue siyo kawaida na inahitaji upate vipimo na tiba hospitali kwani ni kiashiria cha fangasi ukeni.

Uchafu Mwepesi Kama Maji
Uchafu mwepesi kama maji ni kawaida kabisa. Unaweza kupata uchafu huu muda wowote katika mzunguko wako na hasa baada ya kufanya mazoezi.

Uchafu mwepesi unaovutika
Ukiona uteute mwepesi na unavutika kama ute wa yai basi ujue upo kwenye ovulation, yaani siku za hatari na yai limepevuka tayari kwa kurutubishwa. Uteute huu ni wa kawaida.

Uchafu wa brown unaoambatana na damudamu.
Kama unapata uteute huu kabla ya hedhi na ulifanya tendo bila kinga basi kuna uwezekano ukawa umeshika mimba. Kama uchafu huu unatoka wakati mimba yako bado ni changa basi yaweza kuashiria kwamba mimba inaharibika unatakiwa kuwahi hospitali haraka.

Kwa kesi chache sana uchafu wa brown wenye damu damu ni kiashiria cha saratani ya shingo ya kizazi ama pia uvimbe kwenye kizazi(fibroids) ama uvimbe mwingine kwenye kizazi. Ndio maana ni muhimu sana kufanya utrasound kucheki hali ya kizazi endapo utaona dalili zisizo za kawaida kama hizi.

Uchafu Wa njano au kijani
Kama unapata uchafu wa kijani au njano unaoambatana na harufi mbaya siyo jambo la kawaida. Uchafu wa namna hii ni kiashiria kwamba kuna maambukizi ya ugonjwa wa zinaa. Inahitaji uende hospitali haraka kupata vipimo na tiba.

Lini unatakiwa Kumwona Daktari
Kama unapata uchafu usio wa kawaida na unaambatana na dalili hizi muhimu umwone daktari haraka

homa
maumivu chini ya kitovu
kuishiwa nguvu
maumivu wakati wa kukojoa na
kukojoa mara kwa mara


Wasiliana nasi kwa msaada na matibabu mazuri

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data