Description :
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili kama
Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo
Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
Kushindwa kupumua vizuri