Tiba ya Uvimbe Katika Shingo Ya Kizazi (Fibroid)

Tiba ya Uvimbe Katika Shingo Ya Kizazi (Fibroid) - Tanzania
Tiba ya Uvimbe Katika Shingo Ya Kizazi (Fibroid) - Tanzania
  • Tiba ya Uvimbe Katika Shingo Ya Kizazi (Fibroid) - Tanzania
  • Tiba ya Uvimbe Katika Shingo Ya Kizazi (Fibroid) - Tanzania
Description :

Fibroids Ni Kitu Gani? Ni Nini Tiba Ya Fibroids?Fibroids au uvimbe ndani ya kizazi cha mwanamke, ni uvimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha, unaoota na kukua kwenye nyumba ya uzazi (uterus). Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas. Fibroids ni aina ya uvimbe unaoonekana kwa wingi zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Fibroids ni uvimbe ambao mara nyingi (asilimia 99) hauna madhara kiafya na wala kuhusiana na ugonjwa wa kansa.

aina ya fibroids

Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, miaka 30 hadi 50, wana uvimbe katika kizazi (fibroids), ingawa wengi wao hawahangaiki kuchukua vipimo. Uvimbe wa fibroids unakuwa na ukubwa tofauti tofauti, unaweza kuwa mdogo kama haragwe au kufikia ukubwa wa tikiti maji.Chanzo Cha FibroidsSababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen.

Wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa kupata siku zao za mwezi wanaonekana kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids kwa sababu ya kuwa wameishi na homoni ya estrogen kwa muda mrefu zaidi. Wanawake wenye asili ya mchanganyiko wa wamarekani na waafrika (wamarekani weusi) nao wanaonekana kupatwa na fibroids zaidi ya wanawake wengine ingawa sababu bado haijajulikana.

daili za fibroids

Utafiti umeonyesha pia kuwa idadi ya wanawake wanaopatwa na fibroids katika kundi la wanawake ambao wamezaa watoto angalau wawili wakiwa hai huwa ni nusu ukilinganisha na wale ambao hawajazaa hata mara moja. Hapa haieleweki kama kuzaa kulizuia wanawake hawa wasipate fibroids au fibroids ndizo zilizozuia wanawake wa kundi la pili wasizae. Utafiti kuhusu hilli bado unaendelea.Dalili Za FibroidsAkina mama wengine wenye uvimbe wa fibroids huwa hawaoni dalili zo zote zile (wengi hawajui kama wana fibroids) au kuona dalili kidogo na kwa wengine dalili hizi hujitokeza sana na kuwasumbua hadi kufikia kutafuta tiba. Baadhi ya dalili za fibroids ni:

– Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku au kutokwa na damu kwa muda mrefu

– Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku au kutokwa na damu kwa muda mrefu

– Kutokawa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi

– Mauvimu ya nyonga (uvimbe kugandamiza kwenye viungo vya nyonga)

– Kupata haja ndogo mara kwa mara

– Maumivu ya mgongo

– Maumivu wakati wa tendo la ndoa

– Upungufu wa damu kwa sababu ya kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku

– Maumivu ya kichwa

– Maumivu kwenye miguu

– Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa)

– Uzazi wa shida

– Mimba za shida

– Kutopata mimba

– Kutoka kwa mimba mara kwa

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data