Tiba ya ugonjwa wa Pumu

Tiba ya ugonjwa wa Pumu - Tanzania
Tiba ya ugonjwa wa Pumu - Tanzania
  • Tiba ya ugonjwa wa Pumu - Tanzania
  • Tiba ya ugonjwa wa Pumu - Tanzania
Description :

UFAHAMU UGONJWA WA PUMU/ASTHMA
Leo Nina habari njema Kwa wale wote wanaosumbuliwa na pumu kwani suluhusho la matatizo yao limepatikana, hata hivyo napenda tufahamu huu ugonjwa ili tuweze kujikinga na kuwashauri ndugu zetu wenye matatizo haya wapate dawa hiyo.
PUMU AU ASTHMA NI NINI???
-Pumu au asthma ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia ya hewa ambayo huingiza na kutoa hewa katika mapafu
-Ugonjwa huu wa pumu hufanya kuta za ndani ya njia ya hewa kuvimba na hivyo hupunguza kiasi cha hewa kinachoingia na kutoka katika mapafu
- Hali hii husababisha mgonjwa kutoa mlio kama wa filimbi au mluzi wakati wa kupumua pia kubanwa na kifua, kushindwa kupumua vizuri na kukohoa sana
-Watu wenye pumu Mara nyingi hupata Dalili hizo wakati wa usiku na asubuhi sana
-Ugonjwa huu huwaathiri watu wa rika zote ingawaje Mara nyingi huanza utotoni hivyo huwaathiri zaidi watoto
-Ugonjwa huu wa pumu ni mpana sana kwasababu Kuna aina nyingi za pumu kutokana na visababishi vyake
AINA ZA PUMU
1.PUMU YA UTOTONI (CHILD-ONSET ASTHMA)
-Hii ni aina ya pumu inayotokea baada ya mtoto kuwa Kwenye Vizio kama vile VUMBI LA WADUDU KAMA MENDE, MANYOYA YA WANYAMA KAMA PAKA, MBWA PIA KUTUMIA BABY WIPES ZENYE HARUFU (PERFUME)
Pumu hii hutokea kwa kuwa mwili wa mtoto hutengeneza Kinga ya mwili (ANTIBODIES) za IgE zinazosababisha pumu.
Ugonjwa wa pumu ni sugu sana kwa watoto wanaozaliwa na uzito mdogo wenye asili ya kiafrika pia pumu ya utotoni huwaathiri zaidi watoto wa kiume
2.PUMU YA UKUBWANI (ADULT-ONSET ASTHMA)
-Pumu hii huanza baada ya kufika miaka 20, pumu hii huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume na pia haitokei sana kama pumu ya utotoni, Vizio kama vile perfume /cream zenye harufu kali /sabuni nk ndio husababisha pumu hii kwa asilmia kubwa
3.PUMU ITOKANAYO NA MAZOEZI (EXERCISE INDUCED ASTHMA)
-Pumu hii huwatokea Zaidi wanaofanya mazoezi, ikiwa utakohoa na kukosa pumzi wakati wa mazoezi au baada ya mazoezi kuna uwezekano wa wewe kuwa na pumu ambayo inasababishwa na mazoezi pia hata kama sio mwana mazoezi kukimbia kwa kasi angalau dk 10 Kunaweza kusababisha kukosa pumzi kwa muda mrefu na kuonyesha kwamba una pumu
4.PUMU ITOKANAYO NA KUKOHOA SANA (COUGH INDUCED ASTHMA)
-Hii ni aina ya pumu ambayo ni ngumu sana na kuumiza vichwa vya madaktari kuigundua kwasababu katika pumu hii inawezekana isitokee hata Dalili zingine zaidi ya kukohoa kitu ambacho madaktari tunalazimika kuchunguza sababu nyingine za kukohoa sana na kuhakiksha sio zinasababishwa na kukohoa huko
6.PUMU YA USIKU (NOCTURNAL ASTHMA)
-Pumu hii hutokea Kati ya saa Sita usiku na saa mbili asubuhi, pumu hii huamshwa na vumbi la wadudu, rangi ya nyumba, na harufu ya gesi pia Mara nyingi wagonjwa wa pumu hii hushtuka usingizini wakati wa usiku wa manane baada ya kukosa pumzi
7.PUMU KALI ISIYOKUBALI DAWA (SEVERE ASTHMA)
-Wakati wagonjwa wengi wanapata unafuu baada ya kupata steroid wachache hawapati unafuu na hivyo kuhitaji matibabu makubwa Zaidi
8.PUMU YA NGOZI (ECZEMA /ATOPIC DERMATITIS)
-Huenda utashangaa kwamba kuna pumu ya ngozi na ipoje sasa maswali yako yote yamepata majibu, naomba ufahamu kwamba neno ECZEMA ambalo ni neno la kigiriki na linamaanisha KUTUTUMUKA SEHEMU YA NJE YA NGOZI hali ambayo huonekana pale mtu anapopata maradhi haya
-Ugonjwa huu huchangia asilimia 40 ya maradhi yote ya ngozi kwa ufupi huu ugonjwa huwapata Zaidi watoto na tatizo hili limekua likiumiza vichwa vya madaktari na wanasayansi wengi kutokana na kwamba haijajulikana sababu maalum. Ugonjwa huu ni wa muda mrefu nikimaanisha kwamba mtu huweza kukaa na ugonjwa huu kwa muda mrefu ingawa si muda wote mwili huonyesha dalil za ugonjwa huu
CHANZO CHA UGONJWA WA PUMU
-Visababishi vya pumu havijulikani wazwazi ila vitu vinavyochangia pumu ni VIZIO mfano MOSHI WA SIGARA, BANGI, GESI, PERFUME, KUWA NA MSONGO WA MAWAZO, KUOGEA MAJI YA MOTO KILA WAKATI, KUTOKUPAKA MAFUTA, KUKAA KWENYE VUMBI, KUVAA MAVAZI YASIYO YA PAMBA NA KURITHI
DALILI ZA PUMU
-NOTED :Sio watu wote wenye Dalili hizi wana pumu na sio wote wenye pumu Wana Dalili HIZI
��KUKOH

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data