Tiba ya muwasho Ukeni

Tiba ya muwasho Ukeni - Tanzania
Tiba ya muwasho Ukeni - Tanzania
  • Tiba ya muwasho Ukeni - Tanzania
  • Tiba ya muwasho Ukeni - Tanzania
Description :

SABABU YA MUWASHO SEHEMU ZA SIRI..

Kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani bila kujali jinsi, muwasho unaweza kuwa umesababishwa na ugonjwa wa ngozi, zinaa au mzio.

Kuwashwa hutokea pale ngozi inapokereketa ikiambatana na hamu ya kutaka kupakuna. Muwasho huongezeka pale unapokaa na kukiwa na unyevunyevu.

Sababu kuu za kuwashwa kwenye njia ya haja kubwa inaweza ikawa ni sababu fulani kama vile kutojisafisha vizuri baada ya haja, kula vyakula vyenye viungo vingi, kuharisha, vidonda kwenye njia hiyo, maambukizi ya fangasi, bawasiri (hemorrhoids) au minyoo.

Baadhi ya vitu vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi ili kuvikabili. Ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kumuona daktari.

Kwa wanaume
Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanamume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu nyingine za mwili.

Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa, ndio chanzo kikuu cha kuwashwa uume. Sababu nyingine ni maradhi ya fangasi, ugonjwa wa upele (scabies), chawa, mzio na maambukizi ya bakteria.

Kwa wanawake
Kinachosababisha muwasho katika sehemu za siri za mwanamke ni maambukizi ya fangasi ukeni, kuvimba uke wakati wa hedhi na usio wa hedhi, trikomonasi, minyoo, tatizo la shingo ya kizazi, wasiwasi, tatizo la mfumo wa kinga na kisukari.

Maambukizi ya fangasi ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosumbua. Tatizo hili husababishwa na fangasi waitwao Candida. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa.

Ugonjwa wa kuvimba uke kitaalamu unajulikana kama Vulvovaginitis. Ni ugonjwa unaoathiri kwa kusababisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe kuvimba. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, maumivu wakati wa haja ndogo, kukereketa unapokojoa na kutokwa na uchafu ukeni.

Kuvimba uke baada ya hedhi kukoma ama Postmenopausal Atrophic Vaginitis.
Kwa kawaida hutokea baada ya hedhi kukoma. Hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Maambukizi ya trikomonasi. Ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aitwaye trichomonas. Dalili kuu ni muwasho katika uke au uume na kutokwa na uchafu ukeni.

Ugonjwa wa minyoo wajulikanao kama pinworm. Ni maambukizi ya minyoo wadogo wenye umbo la pini wanaoweza kuambukiza kwenye utumbo na kusambaa maeneo mbalimbali. Ugonjwa huu huwatokea zaidi watoto wa kati ya miaka mitano na 10.

Uvimbe wa mrija wa urethra ama kwa kitaalamu urethritis. Ni maambukizi kwenye njia ya kutolea mkojo nje inayoungana na kibofu. Dalili kuu ni mkojo kuchoma, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kutokwa uchafu.

Tatizo la warts. Hivi ni viuvimbe vidogo vinavyotokea juu ya ngozi sehemu za siri.

Vinaweza kuota kama kamba au vimikia vidogovidogo vinavyokua kwa kurefuka. Ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana na husababishwa na virusi vijulikanavyo kama

Human Papillomavirus (HPV). Vivimbe vinaweza kusababisha muwasho na maumivu na hata kuvuja damu vikikandamizwa.
Saratani sehemu ya nje ya uke. Hutokea nje ya uke na kuambatana na hisia za kuwashwa sehemu hizo.

Ugonjwa wa wasiwasi ama Generalized Anxiety Disorder (GAD). unaotokana na hofu ya matukio fulani. Wakati mwingine husababisha kujikuna sehemu mbalimbali hata za siri.

Ugonjwa wa Sjogren. Ni tatizo katika mfumo wa kinga ya mwili unaoathiri tezi zinazosaidia mwili kutengeneza unyevunyevu kwenye macho na mdomo. Ugonjwa huu huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume.

Tatizo la kisukari pia huweza kumuathiri mwanamke sehemu za siri. Ni ugonjwa sugu wa mfumo wa kuzalisha nishati mwilini unaosababishwa na kasoro katika utengenezaji wa insulini au utendaji kazi wake.

Kisukari kilichokomaa kinaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kizunguzungu na kuwashwa sehemu za siri.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data