Tiba ya meno

Tiba ya meno - Tanzania
Tiba ya meno - Tanzania
Tiba ya meno - Tanzania
Tiba ya meno - Tanzania
Tiba ya meno - Tanzania
Tiba ya meno - Tanzania
Tiba ya meno - Tanzania
 • Tiba ya meno - Tanzania
 • Tiba ya meno - Tanzania
 • Tiba ya meno - Tanzania
 • Tiba ya meno - Tanzania
 • Tiba ya meno - Tanzania
 • Tiba ya meno - Tanzania
 • Tiba ya meno - Tanzania
Description :

KUTOBOKA KWA MENO NI NINI?
Kutoboka kwa meno ni ile hali ya jino au meno kutengeneza tundu ikiwa ni matokeo ya asidi (tindikali) izalishwayo na bakteria baada ya mtu kula vyakula vyenye sukari

Nini Kinasababisha Meno Kutoboka?
Meno kutoboka husababishwa na utando asidi (tindikali) izalishwayo na bakteria walioko kwenye utando mlaini ambayo taratibu huweza kutoboa jino husika kwa kuanzia kwenye enameli na kuzidi kuingia ndani zaidi. Kutoboka kwa jino huharibu jino husika ambalo lisipozibwa mapema huweza kuishia kung’olewa.

Enameli Ni Nini? (What is enamel?)
Enameli ni gamba gumu linalofunika jino na ndilo sehemu unayoiona kwenye meno ya mtu yeyote yasiyo na tobo gamba hili ndio kitu kigumu zaidi kuliko chochote katika mwili wa mwanadamu na halina mishipa ya fahamu,damu wala halina hisia za maumivu.

Dentini Ni Nini? (What is dentine?)
Dentini ni gamba la katikati kwenye jino lililoko baada ya enameli, hili ndilo huchukua sehemu kubwa ya jino na kwakua lina na mishipa ya fahamu lina hisia za maumivu. Dentini ndio gamba lililfunika moyo wa jino (pulp).

Je Moyo Wa Jino Ni Nini? (What is the pulp?)
Moyo wa jino ni sehemu laini ya jino ambayo iko katikati kabisa mwa jino na ambyo ina mishipa ya fahamu na mishipa ya damu.
Kwanini Meno Yangu Yanatoboka?
Meno hutoboka wakati sukari iliyopo kwenye chakula inapotumiwa na bakteria walioko kwenye kinywa ambao kisha hutengeneza tindikali (asidi). Kila mara ulapo ama unywapo vitu vilivyo na sukari, tindikali hii hushambulia meno na taratibu huweza kuyatoboa. Mashambulizi haya huweza kuchukua hata saa moja baada ya kuwa umekula vitu vya sukari, kabla ya madini ya chumvi yaliyoko kwenye mate kupambana na hali hiyo. Ikumbukwe kuwa si sukari tu ambayo ni tishio kwa meno yako, hata vyakula vya wanga navyo ni hatari kwani vinaposagwa huweza kutoa sukari ambao nayo huchangia kuozesha meno.
Hivvo basi kutumia vyakula na vinywaji vya sukari kati ya mlo mmoja na mwingine huongeza uwezekano wa kutoboka meno kwani meno husika huwa yanashambaliwa muda wote na yanakosa muda wa kupumzika. Hivyo ni muhimu kujiepusha na matumizi ya vyakula na vinywaji vya sukari kwa siku nzima.

Je Ni Zipi Ni Dalili Za Jino Lililotoboka?
Kwa kawaida kwenye hatua za awali za utobokaji wa meno huwa hakuna dalili yeyote, isipokuwa jino husika huweza kuwa na alama nyeupe kama ya chaki kwenye eneo ambalo linaanza kutoboka. Alama hii huonwa na daktari wa meno anapokuchunguza ama anapopiga mionzi jino husika. Ndio sababu tunasisitiza ni vizuri kumuona Daktari wa kinywa na meno mara kwa mara, tundu dogo ni rahisi kulitibu kuliko tundu lililo kubwa.

Nini Kinatokea Kama Nina Tundu?
Mara tu tundu lililoko kwenye jino linafika kwenye sehemu ya kati ya jino (dentine), jino huanza kuwa na maumivu hasa unapotumia vitu vya baridi au moto, vitu vya sukari ama vya asidi (tindikali).

Nini Kitatokea Kama Sitatibiwa Mapema?
Maumivu ya jino ni dalili kwamba unatakiwa ukamuone Daktari wa kinywa na meno haraka, kwani hiyo huwa ni taarifa kwamba kuna tatizo. Kama usipozingatia madhara yatakua makubwa na inawezekana ukapoteza jino husika ambalo lingeweza kuokolewa kama ungewahi.

Je Ni Maeneo Yapi Ya Meno Huweza Kutoboka Kwa Urahisi?
Maeneo ya kutafunia chakula na maeneo kati ya jino na jino ndio maeneo rahisi zaidi kutoboka, hii ni kwa sababu mabaka ya vyakula na utando mlaini (Plaque) huweza kujishika katika maeneo haya. Lakini kwa ujumla maeneo yote ya meno huweza kutoboka.

Je Nitahitaji Matibabu Ya Aina Gani?
Daktari ataondoa sehemu ya jino iliyooza/toboka na kuweka dawa maalumu ya kujaza eneo husika. Wakati mwingine tundu huwa ni kubwa kiasi cha kuifikia mishipa ya fahamu ya jino husika, inapofikia hapo Daktari huweza kufanya matibabu ya mzizi wa jino ili kuweza kuhakikisha kwamba unaendelea kuwa na jino lako na kulitumia. Na inapotokea kwamba jino lako limetoboka sana kiasi cha kutoweza kukarabatiwa Daktari huweza kushauri kwamba litolewe.

Je Ni Mara Zote Nitahitaji Kuzibwa Meno?
Hapana. Katika hatua za mwanzoni kabisa kama umewahi Dakta

Our safety tips

 • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
 • Never send money to "book" an item, avoid paying before seeing the it.
 • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
 • Thoroughly check the item to make sure it's matching the assumed condition.
 • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
 • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
 • Beware of offers too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data