DALILI/VIASHIRIA VYA UGONJWA WA PID
Kuna dalili mbalimbali zinazoweza kuashiria ugonjwa huu wa PID miongoni mwa dalili hizo ni,
*Mwanamke kupata maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
*Kupata maumivu wakati wa kukojoa
*Kupata homa na kuhisi kichefuchefu
*Kupata maumivu ya mgongo na kutapika
*Kutokwa na hedhi bila mpangilio
*kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
*Kutokwa na uchafu(utoko)mweupe ukeni unaotoa harufu mbaya
NAMNA YA KUJIEPUSHA NA UGONJWA WA PID
Pamoja na kuwepo kwa dawa za kutibu tatizo hili ni vyema ukajiepusha na vihatarishi vya kupata tatizo hili kwa kuzingatia yafuatayo,
*Epuka kufanya ngono isiyo salama.
*Jiwekee tabia ya kufanya vipimo mara kwa mara hasa kizazi
*Usifanye mapenzi mara baada ya kujifungua au mimba kutoka mpaka utakapohakikisha shingo ya uzazi imefunga vema
*Kuwahi kuonana na daktari unapoona dalili za ugonjwa
*Kuwa msafi na kula lishe bora
Tiba ya maambukizi katika via vya uzazi(PID)
Description :
This listing was not posted by a representative of Jumia. Jumia cannot guarantee the origin of the product / service.