TIBA YA KUZIBUA MIRIJA YA UZAZI/FALLOPIAN TUBE

TIBA YA KUZIBUA MIRIJA YA UZAZI/FALLOPIAN TUBE - Tanzania
  • TIBA YA KUZIBUA MIRIJA YA UZAZI/FALLOPIAN TUBE - Tanzania
Description :

CHANZO CHA KUZIBA MIRIJA YA UZAZI....✍️?✍️?✍️?

Kuziba kwa mirija ya uzazi ni moja ya sababu inayochangia ugumba kwa wanawake, mirija hii hujulikana kitabibu kama Fallopian tube ndiyo inayounganisha kokwa za kike (ovary) na nyumba ya uzazi....
Kuziba kwa mirija ya uzazi ni moja ya sababu inayochangia ugumba kwa wanawake, mirija hii hujulikana kitabibu kama Fallopian tube ndiyo inayounganisha kokwa za kike (ovary) na nyumba ya uzazi.

Kila mwezi katikati ya mzunguko wa hedhi kijiyai huchoropoka na kusafiri kutoka katika kokwa za kike kupitia katika mirija ya uzazi na kwenda katika nyumba ya uzazi.

Endapo mbegu ya kiume itarutubisha kijiyai cha kike katika mirija muunganiko huo husafiri na kujipachika katika tando nyororo za nyumba ya uzazi kwa ajili ya kupiga hatua za ukuaji (mimba).

Kama mirija hii itazibwa kwa namna yoyote ile ina maana kuwa mbegu za kiume zitashindwa kwenda kurutubisha kijiyai cha kike.

Ni kawaida pia mirija kuziba na kuacha kipenyo hivyo mbegu ya kiume hupita na kupandikiza kijiyai lakini baadaye hushindwa kusafiri kwenda katika nyumba ya uzazi kwa ajili ya mimba kukua.

Zipo sababu mbalimbali ambazo zinachangia mara kwa mara kujitokeza kwa tatizo hili ikiwamo uwepo wa kovu, maambukizi na kukandamizwa na tishu za maeneo ya kiunoni.

Maambukizi ya bakteria katika viungo vilivyopo ndani ya kiuno ikiwamo nyumba ya uzazi hushambuliwa na kusababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi.

Makovu hayo kutokana na maumbile yake huweza kusababisha kijiyai kukwama. Uwepo wa tatizo la tishu za tando laini za nyumba ya uzazi kujirundika eneo lisilo lake ikiwamo katika mirija ya uzazi husababisha kuziba, tatizo lijulikanalo kitabibu kama Endometriosis.

Vile vile tishu hizo huweza kujipachika nje ya nyumba ya uzazi na kubanana na mirija hiyo na hatimaye kuiziba.

Magonjwa yanayoenea kwa njia ya kujamiiana ikiwamo kisonono (Gonorrhea) na klamidia hushambulia maeneo ya viungo vya uzazi hivyo kuchangia tatizo hili.

Kuwahi kufanyiwa upasuaji baada ya mimba kutunga na kukua katika mirija badala ya nyumba ya uzazi (Ectopic Pregnancy) upasuaji huu huweza kuacha kovu katika mirija.

Uvimbe wa Fibroid unaweza kuwa mkubwa na kuziba katika mirija hiyo hasa mahala ulipojichimbia katika nyumba ya uzazi.

Kuwahi kufanyiwa upasuaji wa nyumba ya uzazi hasa katika mirija yenyewe inaweza kusababisha kushikamana na tishu za tumbo na mirija hiyo kuziba.

Mambo mengine hatarishi ni pamoja na vimelea kushambulia katika nyumba ya uzazi, kuharibika kwa mimba mara kwa mara na kujifungulia maeneo yasiyo salama.

Madhara ya kuziba ni pamoja na mimba kutungwa na kukua katika mirija tatizo linaloitwa Ectopic Pregnancy, hutokea baada ya mbegu za kiume kupita katika upenyo wa mrija ulioziba kwa kiasi. Madhara makubwa ni pale mirija yote miwili inapokuwa imeziba bila kuacha upenyo wowote hivyo mbegu ya kiume hushindwa kupita kwenda kuungana na kijiyai cha kike. Matokeo ya hali ni kupata ugumba kwa wanawake.

TIBA NA USHAURI.
Kuondoa Uchafu/Maji maji katika mirija/Kuzibua mirija itahitaji matibabu ambayo yatatolewa na mtaalamu baada ya kujua chanzo cha hali hiyo kutokea kwani kama tulivyoona hapo juu, sababu za tatizo hili zipo nyingi.Pia tunazo dawa za asili/naturalCeutical utakazotumia kumaliza tatizo lako baada ya kupata ushauli wa daktari.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data