Tiba Ya Bawasiri Sugu.

Tiba Ya Bawasiri Sugu. - Tanzania
Tiba Ya Bawasiri Sugu. - Tanzania
  • Tiba Ya Bawasiri Sugu. - Tanzania
  • Tiba Ya Bawasiri Sugu. - Tanzania
Description :

Bawasiri Husababishwa Na Nini?Sababu kamili inayofanya mabadiliko madogo yatokee kwenye veni zilizoko kwenye utando unaofunika anal canal na kusababisha bawasiri kutokea haijafahamika. Bawasiri nyingine hutokea bila sababu maalumu. Inafikirika kuwa kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye eneo la ndani na linalozunguka tundu la haja kubwa kunaweza kuwa ndiyo sababu kubwa.

Kuna mazingira yanayochangia uwezekano wa kutokea kwa bawasiri kuwa mkubwa zaidi, nayo ni:

Kufunga Choo: Kutoa kinyesi kikubwa au kujikamua kwa nguvu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Hii huongeza msukumo ndani na kuzunguka veni za kwenye tundu la haja kubwa. Hii inaonekana kuwa ni sababu kubwa ya bawasiri kutokea.bawasiri chanzoMimba: Ni kawaida kabisa bawasiri kujitokeza wakati wa uja uzito. Hii labda hutokea kutokana na msukumo unaotokea juu ya rectum na anus kwa kutokana na mtoto kulalia juu ya maeneo hayo na kutokana na matokeo yanayotokana na mabadiliko ya homoni wakati wa uja uzito kwenye veni..

Kuzeeka: Tishu zinazozunguka ndani ya mkundu zinaweza kupoteza nguvu zake kadri umri unavyokuwa mkubwa.

Kurithi: Watu wengine wanaweza kurithi udhaifu wa kuta za veni za kwenye eneo la tundu la haja kubwa.

Sababu nyingine zinajumuisha kunyanyua vitu vizito na kikohozi cha muda mrefu (sugu).
Dalili Za Bawasiri.Dalili za bawasiri hutofautiana. Wakati mwingine hakuna dalili zinazojitokeza na mtu anaweza asijue kuwa ana bawasiri.

Dalili ya kawaida kabisa ni kutokwa na damu wakati ukienda kujisaidia haja kubwa. Damu huonekana iliyo mbichi, nyekundu, juu ya toilet tissue, kwenye sahani ya choo au ikiwa imekizunguka kinyesi.

Bawasiri huweza kuchomoza na kuning’inia nje. Mara nyingi unaweza kuzisukuma na vidole zikarudi ndani baada ya kujisaidia. Lakini bawasiri zilizofikia hali mbaya huning’inia moja kwa moja nje na huweza kuzisukuma ndani.

Bawasiri ndogo za ndani kwa kawaida hazina maumivu. Bawasiri kubwa huweza kutoa majimaji, kuwa na maumivu, na kuwasha. Majimaji yatokayo yanaweza kuchubua eneo linalolizunguka tundu la haja kubwa. Unaweza kuwa na hisia za kuwa na haja kubwa au kuwa hujamaliza vizuri haja zako ukiwa unatoka msalani.

Matokea mabaya ya bawasiri zinazoning’inia ni kuwa zinaweza zikajifinyanga na kusababisha damu kushindwa kupita kuelekea kwenye bawasiri hizo, hali ambayo inaweza kuleta maumivu makali sana. Mara chache inaweza ikatokea kuwa damu ikaganda ndani ya bawasiri (thrombosis) hizo, hali ambayo huleta maumivu makali pia.


Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data