TIBA YA BAWASIRI

TIBA YA BAWASIRI - Tanzania
  • TIBA YA BAWASIRI - Tanzania
Description :

Bawasiri yaweza kuwa moja ya topic ngumu sana kuzungumziwa kiuwazi na watu, hii ni kutokana na wagonjwa wengi kuona aibu pengine ni kwasababu tatizo husika hutokea mahala pa haja kubwa. Wengine huona aibu hata kueleza tatzo hili kwa Dactari ama muhudum wa afya, bawasili ni tatizo kuwa linawatokea wanaume kwa wanawake. Naweza kusema uwepo wa tatizo hili si ajabu ukianagalia wengi wetu wanakula vyakula zaidi vilivyosindikwa, hawafanyi mazoezi na wana msongo wa mawazo uliokithiri.

Je, Unajua Bawasiri/Hemorrhoids Ni Nini?
Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe. Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS na kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles.

Tatizo la bawasili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50% ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 40 mpaka 50.

Aina Za Bawasiri
Kuna Aina kuu mbili za bawasiri

(A) Bawasili ya ndani
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili,.Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa

Aina hii imegawanyika katika madaraja manne

(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika

(2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.

(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.

(4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi.

(B)Bawasili ya nje

Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS

Nini Chanzo Cha Bawasiri?

Bawasili kwa kiasi kikubwa huletekezwa na kuongezeka kwa mganadamizi ama presha mara nyingi ni pale unapojikaza ili kutoa haja kubwa. Hivo bawasili huwatokea zaidi watu wenye matatizo ya mfumo wa umen’gemnyaji mfano unapata choo kigumu, tumbo kujaa gesi, kukosa choo kwa siku kadhaa. Wamama wenye ujauzito pia huwa kwenye hatari kubwa ya kupata bawasili kutokana na mtoto aliye tumboni kugandamiza tumbo la chakula na hivo kuathiri utoaji wa haja kubwa, kwa bahati nzuri bawasili inayosababishwa na ujauzito huanza kuisha pale tu mama anapojifungua. Watu wenye kitambi na uzito mkubwa pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata bawasili kutokana na mwili kushindwa kutengeneza nishati ya kutosha kusukuma uchafu kwenye utumbo.

Unagunduaje Kama Tayari Una Bawasiri
wakati mwingine inatokea unaweza kuwa na bawasili lakini usipate dalili na baada ya mfupi ugonjwa huweza kupotea wenyewe. Dalili moja kubwa ambayo wagonjwa wetu wengi huipata kwa wenye bawasili ya ndani ni kuvuja kwa damu inatyoweza kuonekana kwenye toilet paper ama kinyesi, unapoona dalili kama hizi hakikisha unachukua hatua za haraka maana tayari umepata bawasiri. Kama una bawasiri ya nje basi unaweza kupata viashiria kama uwepo wa nundu nyekundu iliyojaa damu pembeni mwa mahala pa haja kubwa, kitaalamu huitwa thrombosed hemorrhids na huambatana na maumivu makali sana wakati wa kutoa haja, kama utoaji wako wa haja ni wa kujikamua na kwenda haraka haraka, na kujisafisha kupita kiasi basi unaweza kuongeza tatizo, ianashauriwa kutotumia nguvu kubwa kujisaidia.

Angalizo (Siyo Kila Unapoona Kuna Damu Inavuja Ni Bawasili)
Unapoona kuna damu inavuja mahala pa haja kubwa ama unapotoa haja, basi nashauri nenda haraka hospital kuonana na Dactari na kufanya vipimo, hasa kama tatizo ni limekutokea kwa mara ya kwanza.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data