Tatizo ya kupata hedhi nyingi kupita kiasi

Tatizo ya kupata hedhi nyingi kupita kiasi - Tanzania
  • Tatizo ya kupata hedhi nyingi kupita kiasi - Tanzania
Description :

TATIZO LA KUPATA HEDHI NYINGI KUPITA KIASI ( HEAVY MENSES ), SABABU NA ATHARI ZAKE KWENYE AFYA
Kupata hedhi kupita kiasi ni moja ya matatizo ya uzazi yanayosumbua wanawake wengi. Tafiti zimeonyesha kwa kila wanawake 1000; wanawake 53 kati ya huwa na tatizo la kupata hedhi kupita kiasi. Ni theruthi tu ya wanawake wenye shida ya hedhi hutafuta tiba stahiki kwa daktari wengi hukaa nayo kwa aibu au hofu.
Makala hii nimegusia katika lugha rahisi visababishi vya hedhi kutoka nyingi ili itoe mwanga kwa wanawake kutafuta tiba pale wanapokabiriwa na changamoto hii
Je ni wakati gani mwanamke anatakiwa kuhisi kuwa anapata hedhi kupita kiasi?
Unapata hedhi inayozidi siku 7
Unapata hedhi nzito inayofanya ubadiri pedi moja ndani ya masaa mawili
Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuvaa pedi zaidi ya moja
Unapata hedhi nzito inayolowesha hadi nguo za nje
Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuamka usiku kubadiri pedi
Hedhi inayotoka na mabonge
Sababu gani huweza kuchangia mwanamke kupata hedhi nzito kupita kiasi?
Vivimbe kwenye kuta za mji wa kizazi; vivimbe hivi sio saratani huitwa fibroids
Yai kupevuka bila mpangilio (Irregular ovulation) ; hali hii husababisha kuta za mji wa mimba zivimbe na kuwa nene hivyo kutoa damu nyingi. Hutokea zaidi kipindi cha kuvunja ungo na kipindi cha kukaribia ukomo wa hedhi
Matatizo ya kugandisha damu
Matumizi ya dawa za kuzuia damu kuganda
Baadhi ya wanawake waliotumia vitanzi (IUD) hasa ndani ya mwaka wa kwanza
Maambukizi ya mji wa mimba na mirija ya uzazi (PID)
Endometriosis
Saratani ya mji wa kizazi; kwa kinamama waliofikia umri wa ukomo wa hedhi. Wakianza kupata hedhi isiyokoma huweza kuwa dalili ya ya saratani ya mji wa kizazi
ATHARI ZA HEDHI NZITO KUPITA KIASI KWENYE AFYA
Hedhi nzito kupita kiasi huchangia wanawake wengi kupata upungufu wa damu
Hedhi kuwa nzito kupita kiasi huweza kuwa ni dalili ambao unahitaji tiba ya haraka
Huweza kuchangia kudhoofisha afya ya akili ya mwanamke ikiwemo kujiamini na wasiwasi

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data