TATIZO LA STROKE/KIHARUSI NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA STROKE/KIHARUSI NA MATIBABU YAKE - Tanzania
  • TATIZO LA STROKE/KIHARUSI NA MATIBABU YAKE - Tanzania
Description :

Kiharusi ni hali inayotokea pale mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo inapopatwa na misukosuko kiasi cha kushindwa kupeleka damu kwenye ubongo na hivyo kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo kwa zaidi ya masaa 24.

Kiharusi kimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea "visababishi vyake". Aina hizo ni
- Kiharusi cha kukosa hewa kwenye Ubongo (Ischemic stroke) ,Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kupelekea tishu za ubongo za eneo liliathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri Aina hii ya kiharusi husababishwa naDamu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo "cerebral thrombosis" au​
Kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo "cerebral eembolisms"

-Kiharusi Cha kuvuja damu ndani ya Ubongo "Haemorrhagic Stroke"
Aina hii ya kiharusi hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu ndani ya ubongo hupasuka na kusababisha kusambaa kwa damu ubongoni "cerebral hemorrhage". Mara nyingi aina hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma, au kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa.​

Visababishi vya Kiharusi kwa ujumla.
Wakati fulani, mishipa ya damu huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwili, hali inayoitwa kitaalamu kama atherosclerotic plaque. Hali hii husababisha kuganda kwa damu katika mishipa "thrombosis" hiyo. Kuganda huku kwa damu kunaweza kutokea kwenye mishipa mikubwa au midogo inayopeleka damu kwenye ubongo. Baadhi ya mishipa mikubwa ya damu inayoweza ​kuathirika na tatizo hili ni pamoja na arteri za common carotid na interior carotid arteries, na arteri za vertebral. Nyingine ni mishipa midogo inayounda eneo linaloitwa circle of willis lililo katika ubongo.​

Kuganda kwa damu (embolus) kwenye mishipa ya damu ya sehemu nyingine za mwili au "hewa, mafuta, kusanyiko la vijimelea kama bakteria waletao ugonjwa wa endocarditis" huweza kusababisha kuziba kwa mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo kusababisha kiharusi.

Upungufu wa usafirishaji damu mwilini "systemic hypoperfusion" Wakati fulani moyo hushindwa kusukuma damu vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo ubongo kutokana na kufa kwa sehemu za nyama ya moyo kwa kukosa damu ya kutosha "Ischaemic Heart Diseases" au kutokana na kujaa kwa maji kwenye gamba lake la nje "pericardial effusion"au kupungua kwa damu mwilini.

Shinikizo la damu la muda mrefu lisilothibitiwa linaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa midogo inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo damu kujaa kwenye ubongo "Intracerebral hemorrhage"

Dalili za kiharusi hutegemea na eneo la ubongo liliathiriwa
Iwapo sehemu ya ubongo mkubwa " Cerebellum" itaadhirika, mgonjwa atakuwa na dalili kama kushindwa kutembea vizuri, hivyo kuathiri mwendo wake, kujihisi kizunguzungu maumivu ya kichwa, kutapika na kupoteza fahamu
Aidha bila kujalisha eneo lililoathiriwa, mgonjwa pia anaweza kuwa na dalili za kupoteza fahamu, maumivu makali ya kichwa na kutapika. Dalili hizi za kuumwa kichwa na kutapika kwa kawaida hutokea kwa mgonjwa mwenye kiharusi cha kuvuja damu "hemorrhagic stroke" ambacho husababisha ongezeko la shinikizo na mgandamizo wa ubongo ndani ya fuvu la kichwa.

Vitu vinavyoweza kumuweka mtu katika hatari ya kupata kiharusi ni pamoja na kisukari, uvutaji sigara, unywaji pombe kupita kiasi ,unene na uzito ,kutoshuulisha mwili,kuwa na lehemu nyingi Katika Damu nk,

Unapogundulika na Tatizo Hili Unashauriwa kuonana na Daktari kwa ajiri ya Vipimo vya mionzi MRI,CT- scan,PET, SPECT na vipimo vingine Kama ECHO, Kisha utapatiwa Matibabu na management zingine.

Pia tunayo tiba maalumu Naturalceutical, dawa zisikuwa na chemikali ambazo husaidia kuondoa lehemu na UVimbe "tumors" katika ubongo, kujenga blood vessels zilizopasuka na hivyo kuruhusu Damu yenye virutubisho Mhimu na hewa Safi ya Oxygen kusambaa vizuri katika tissue za ubongo na sehemu mbali mbali za Mwili na hivyo kufanya afya ya mgonjwa kuimarika Zaidi.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data