Tatizo la ugumba kwa mwanamke

Tatizo la ugumba kwa mwanamke - Tanzania
Tatizo la ugumba kwa mwanamke - Tanzania
Tatizo la ugumba kwa mwanamke - Tanzania
  • Tatizo la ugumba kwa mwanamke - Tanzania
  • Tatizo la ugumba kwa mwanamke - Tanzania
  • Tatizo la ugumba kwa mwanamke - Tanzania
Weka maudhui :

*SABABU ZA MWANAMKE KUTOKUSHIKA MIMBA*
Kwa kawaida mwanamke anatakiwa apate ujauzito ndani ya mwaka mmoja baada tu ya kuolewa au kuanza uhusiano. Tunategemea baada ya miaka miwili hadi mitatu baada ya kupata mtoto apate mwingine labda kama hajaamua yeye pamoja na mumewe. Ujauzito unapatikana baada ya kufanya tendo la ndoa kwa ukamilifu, yaani katika kipindi ambacho mwanamke anaweza kupata ujauzito (siku za hatari).
Swala hili pia linaangalia kwa upande wa pili wa mwanaume ambaye pia tunategemea ana uwezo huo wa kumpa mwanamke mimba kwa kuwa na mbegu zenye ubora na nyingi, pia awe na nguvu za kutosha za kufanya tendo ili mwezi wake apate ujauzito. (Kuhusu mwanaume tayari somo lake).
*ZIPO AINA MBILI ZA KUTOSHIKA MIMBA (INFERTILITY)*
1.AINA YA KWANZA (PRIMARY INFERTILITY)
Hii ni kwa wale ambao mke na mume hawakuwai kubahatika kupata mtoto hata mmoja tangu waoane au wawe kwenye mahusiano ili hali wanakutana kimwili bila kutumia kinga yoyote Ile.
2.AINA YA PILI (SECONDARY INFERTILITY)
Hii ni kwa wale ambao mke na mume walishazaa mara moja Lakini hawafanikiwi kupata mtoto mwingine ili hali wanakutana kimwili bila kutumia kinga yoyote.
*VITU VINAVYOSABABISHA MWANAMKE KUSHINDWA KUPATA MIMBA NI;*
1.Kutokuwa na uwiano mzuri wa homoni (Hormonal Imbalance)
2.Ovaries kushindwa kutoa mayai
3.Kuziba kwa mirija ya uzazi
4.Mirija ya uzazi kujaa maji
5.Uvimbe katika kizazi (uterine fibroid)
6. Magonjwa kama vile PID, kisonono kisukari nk
7.Kuwa na msongo wa mawazo
8.Utoaji wa mimba (Abortion)
9.kuwa na uzito kupita kiasi (over-weight)
10.Matumizi ya pombe, bangi, sigara, ulevi kupindukia
11.Matumizi ya madawa
12.Endometriosis:-Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuota nje ya fuko hilo au hata sehemu nyingine.
Hizo hapo ni baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha mwanamke asipate ujauzito.
*DALILI*
1.Mwanamke anayesumbuliwa na maumivu chini ya tumbo mara kwa mara naye yupo katika hatari hii kwani upo uwezekano wa kuathiri mirija yake ya uzazi na ikaziba kabisa, mzunguko wa hedhi unavurugika na kupoteza hamu ya tendo la ndoa
2.Wanawake wengine hupata maumivu ya kiuno na tumbo kwa muda mrefu sio dalili nzuri, matiti au chuchu kutoa maziwa pia huathiri kwa kiasi kikubwa uzazi na inakua vigumu kupata ujauzito hasa kwa wasichana
3.Maumivu wakati wa hedhi pia si dalili njema katika mfumo wa uzazi kwani inaweza kuwa una maambukizi sugu ya kizazi (chronic pid), uvimbe katika kizazi (uterine fibroid) na nyinginezo.

Vidokezi vyetu vya usalama

  • Matangazo yaliyo na neno "Duka" yametolewa na Jumia.
  • Epuka kulipa chochote kabla ya kuonyeshwa bidhaa
  • Epuka kutuma pesa kwa njia zisizofuatilika kama vile Western Union au Pesa za Simu
  • Tazama kabisa unachokinunua, uhakikishe kuwa liko katika hali iliyotajwa kwenye tangazo
  • Kama muuzaji hana duka, kutane naye mahali pa umma (Mall, kituo cha gesi, mahali pa kazi ...)
  • Usipatiane maelezo yoyote ya kibinafsi (maelezo ya benki, nambari za kadi ya mkopo ...).
  • Jihadhari na bei zisizoaminika kuwa za ukweli.

Bidhaa gani unayo ya kuuza?

Uza kila kitu bure kupitia Jumia Deals.co.tz

Weka tangazo lako bure kuanzia sasa!
Tunasindika taarifa