JINSI YA KUONDOKANA NA UVUMBA KWA MWANAMKE

JINSI YA KUONDOKANA NA UVUMBA KWA  MWANAMKE - Tanzania
  • JINSI YA KUONDOKANA NA UVUMBA KWA  MWANAMKE - Tanzania
Weka maudhui :


Ugumba ni tatizo linaloathiri takribani mmoja kati ya wanandoa 6. Utambuzi wa ugumba unakamilika pale wanandoa wanapojaribu kupata mtoto kwa mwaka mzima bila mafanikio.

NI NINI CHANZO CHA UGUMBA KWA MWANAMKE?

Sababu kuu ya ugumba inahusisha matatizo ya yai kupevushwa, kuharibika mirija ya falopiani au mfuko wa uzazi(uteras), au matatizo ya mlango wa uzazi(cervix). Umri unaweza changia pia, kadiri mwanamke anavyokua kiumri ndivyo uwezo wake wa kupata ujauzito unapungua.

TATIZO LA KUPEVUKA YAI LINASABABISHWA NA MAMBO YAFUATAYO:

Mabadiliko ya homoni
Uvimbe au jipu kwenye mfuko wa mayai
Matatizo katika mfumo wa ulaji, mfano anorexia nervosa (albamu) au bulimia nervosa.
Matumizi ya pombe au madawa ya kulevya
Matatizo ya tezi ya thairoidi.
Uzito uliopitiliza
Msongo wa mawazo
Mazoezi makali ya mwili yenye kusababisha upungufu wa mafuta mwilini uliopitiliza.
Mzunguko mfupi wa hedhi.
Matatizo ya uharibifu wa mirija ya falopiani au mfuko wa uzazi (uterasi) unaweza kusababishwa na yafuatayo:

Uvimbe kwenye nyonga.
Maambukizi ya nyonga yaliyopita.
Ugonjwa wa “endometriosis” au uvimbe katika mfuko wa uzazi.
Uvimbe wenye maji ndani ya mfuko wa uzazi unaosababishwa na “endometriosis”.
Kovu kwenye mfuko wa uzazi au “adhesion” ( kushikana kwa tishu wakati wa kushonwa kidonda baada ya upasuaji).
Ugonjwa wa kudumu.
Tatizo lililopita la mimba kutungwa nje ya mji wa mimba.
Kasoro ya kuzaliwa
DES syndrome (dawa, iliyotolewa kwa wanawake ili kuzuia kupoteza mimba au mtoto kuzaliwa mapema kabla ya wiki ya 37 inaweza kusababisha matatizo ya uzazi.)
Uteute usio wa kawaida kwenye mlango wa kizazi unaweza pia kusababisha ugumba. Uteute usio wa kawaida ndani ya mlango wa kizazi unaweza kuzuia mbegu za kiume kufika kwenye yai au kufanya ugumu wa mbegu za kiume kupenya na kuingia kwenye yai.

MWANAMKE MGUMBA UNATAMBULIKAJE?

Ugumba kwa mwanamke hupimwa kama sehemu ya uchunguzi wa mwili.Vipimo vinahusisha uelewa wa matibabu ya zamani na mambo yanayoweza kuchangia ugumba.Jinsi gani ugumba unatibika?

UGUMBA KWA MWANAMKE UNATIBIWA KWA NJIA ZIFUATAZO:

Matumizi ya vidonge vya homoni ili kurekebisha mabadiliko ya homoni, “endometriosis” au mzunguko mfupi wa hedhi.

Matumizi ya dawa za kuchangamsha upevushwaji wa yai
Matumizi ya virutubisho vya kuongeza uwezo wa kupata ujauzito (vya kununua).

Matumizi ya antibaiotiki za kuondoa maambukizi ya magonjwa ya ngono.
Upasuaji mdogo kutoa aina yoyote ya makovu ya tishu ndani ya mfuko wa uzazi na uzibaji kwenye mirija ya falopiani,uterasi au eneo la nyonga.

Kwa ujumla ugumba ndo tishio katika ndoa nyingi na asilimia kubwa ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu mmoja wao ana tatizo hili hivyo kama ungependa kupata elimu njia mbadala ya kuepukana na ugumba kwa mwanamke na pia hata kwa mwanaume comment hapo chini upate elimu bure na ushauri pia kuondoa au kukabiliana na ugumba.

Bidhaa gani unayo ya kuuza?

Uza kila kitu bure kupitia Jumia Deals.co.tz

Weka tangazo lako bure kuanzia sasa!
Tunasindika taarifa