Karibu Huduma kwa Wateja ya Jumia Deals.co.tz

Hapa tutakupatia majibu katika maswali yanayoulizwa mara kwa mara na njia za kuuza na kununua kwa kwa haraka na Usalama.

Jinsi ya Kuuza Simu Yako ya Mkononi

Ukiwa unatangaza Simu Yako ya Mkononi kwenye tovuti ya Jumia Deals.co.tz, utaona kwamba tangazo lako liko sawa tu na nyingine zilizoko. Huu ni ushauri wetu kukusaidia uuze Simu Yako ya Mkononi haraka:

Weka Picha

Watu wengi watakao tafuta kupitia mtandaoni watavutiwa na bidhaa yenye picha "matangazo yenye picha". Hakikisha kwamba picha yako ni safi, piga picha yako kukiwa na mwanga wa kutosha kisha weka picha nyingi (haswa kuonyesha jina la bidhaa na sehemu wapi imeharibika kama ipo).

Kuwa Wazi Kuhusu Sehemu Wapi Imeharibika na Hali ya Kifaa Chako

Usisahau kwamba Jumia Deals.co.tz ni soko la vitu ambavyo vimeshatumika. Wanunuzi wanaheshimu ukweli kuhusu hali ya kifaa chako, hivyo usisahau kutaja sehemu zilizo haribika kwa maelezo au uonyeshe kwa picha.

Weka bei inayofaa

Kupata mwelekezo wa bei ya simu yako, tafuta vifaa vingine kama hivyo kwenye tovuti yetu kwenye sehemu unayoishi. Kwa kuipa bei inayofaa, utaweza kuuza simu yako papo hapo.