Karibu huduma kwa Wateja ya Jumia Deals.co.tz

Hapa unaweza kupata majibu kwa maswali ambayo yanaulizwa mara kwa mara pamoja na kujifunza jinsi ya kuuza na kunua kwa haraka na usalama.

Jinsi ya Kuuza Nyumba Yako

Kama ungependa kuuza nyumba au kiwanja chako kupitia Jumia Deals.co.tz na hujui jinsi ya kufanya hivi, fuata maelekezo yetu na ushauri wetu.

Andika maelezo yanayojitosheleza

Maelezo ya kujitosheleza ni utambulisho wa nyumba yako, inamfanya mteja kupata sura kamili ya ubora wa bidhaa yako. Hakikisha unaelekeza eneo au mtaa, Ukubwa wa eneo, idadi ya vyumba na uwezo wake.

Kutathmini mali yako kwa usahihi

Inashauriwa sana kutafuta wajuzi wa masuala ya nyumba. La sivyo unaweza pia kutathmini bei za matangazo yaliyo kwenye tovuti na kufananisha na bidhaa yako, fikiria kwa umakini katika eneo la nyumba yako na bora wake. Kama bei yako ipo juu zaidi, unaweza kupata shida kupata mteja.

Weka picha

Picha za kuvutia kwenye tangazo lako. Kuwafanya watu watake kununua mali yako, ionyeshe kwa sifa zake zote nzuri. Piga picha nyingi na kuzirusha zote ambazo ni nzuri, za vyumba vyote na sehemu zote za nyumba hiyo. Jaribu kutumia kamera ya dijitali kupata picha bora zaidi.