Karibu huduma kwa Wateja ya Jumia Deals.co.tz

Hapa unaweza kupata majibu kwa maswali ambayo yanaulizwa mara kwa mara pamoja na kujifunza jinsi ya kuuza na kunua kwa haraka na usalama.

Jinsi ya Kuuza Gari Lako

Huu ni ushauri wetu kukusaidia uuze Gari lako kwa haraka.

Uza kwa bei Nzuri

Kuna vitu vingi ambavyo vitavutia katika kupanga bei ya gari lako, hivyo kagua matangazo kama ya bidhaa yako na angalia vitu kama vile (aina ya enjini, aina la gari na mileage) kupitia tovuti ya vendito ili kupata idea ya thamani ya gari yako. Kumbuka kuwa kuuza gari yako katika bei nafuu na ya makubaliano itafuvutia wateja wengi zaidi.

Picha

Inapendekezwa kwamba uweke picha nyingi, kuonyesha pande zote, kwa ndani, na kuweka picha za enjini. Hii imeshaonyesha kuwavutia wateja na kujenga uaminifu kwao.

Maelezo

Andika maelezo ya kina ya gari lako na hakikisha unataja kila aina ya ubora wake na Kama gari lako linavifaa vingine( AC, ABS, Power Steering n.k...). Kitu flani kinaweza kikawa cha kawaida kwako wewe lakini kumbe ni cha muhimu sana kwa Mteja.
Kuweka uaminifu kwa wateja, elezea sababu za wewe kuuza gari lako: labda ni kwa sababu umepata gari kwenye kampuni unayofanyia kazi, unahitaji gari kubwa zaidi, unasafiri kwenda nje au sababu unahitaji pesa tu.

Njia muhimu kwa wateja

  • Hakikisha kwamba mwuzaji ni mmiliki wa gari hilo.
  • Hakikisha kwamba ukague asili ya gari hilo kabla hujalinunua (hakikisha kwamba siyo gari ambalo limeibiwa).
  • Kagua mwongozo wa matengenezo ujuwe ukweli wa mileage ya gari hilo.
  • Pia hakikisha kwamba umeangalia kadi ya gari kutoka mamlaka bado ni ya halali.
  • Hakikisha kwamba gari linaguliwa na fundi ambaye siyo wa mwuzaji.
  • Hakikisha kwamba msaini mkataba wa mauzaji.