Karibu huduma kwa Wateja ya Jumia Deals.co.tz

Hapa unaweza kupata majibu kwa maswali ambayo yanaulizwa mara kwa mara pamoja na kujifunza jinsi ya kuuza na kunua kwa haraka na usalama.

Jinsi ya Kuuza Haraka

1. Chagua bei inayofaa

Kuchagua bei inayoendana na kifaa chako unaweza kukagua matangazo mengine kama hilo lako kwenye tovuti yetu na kuchagua bei nafuu zaidi.

2. Andika maelezo ya kifaa chako

Maelezo mazuri ya kifaa chako itamrahisishia mteja aelewe ni nini ambacho unakiuza. Hakikisha kwamba jina ambalo unaloliweka ni fupi na sahihi.

3. Tangazo lenye picha linauza haraka zaidi kwa mara 7!

Pamoja na maelezo yako, weka picha moja au zaidi za kifaa chako kuonyesha pande zote. Hii itahakikisha bidhaa yako iuzike haraka.