Karibu huduma kwa Wateja ya Jumia Deals.co.tz

Hapa unaweza kupata majibu kwa maswali ambayo yanaulizwa mara kwa mara pamoja na kujifunza jinsi ya kuuza na kunua kwa haraka na usalama.

Maswali ya mara kwa mara

Kuhusu Jumia Deals.co.tz

Jumia Deals.co.tz ni nini?
Jumia Deals.co.tz ni tovuti ya matangazo madogo madogo ambayo inakupa fursa ya kuweza kununua na kuuza kila aina ya bidhaa katika sehemu unayoishi – inachukua muda wa dakika 2 tu kurusha tangazo lako na ushiriki wako kwa 100% ni bure!
Ni Bure kutumia Jumia Deals.co.tz?
Ndiyo, Jumia Deals.co.tz kwa 100% ni BURE na itakuwa hivyo siku zote.
Inabidi nijisajili kutumia Jumia Deals.co.tz?
Unaweza kukagua na kurusha matangazo yako kwenye tovuti ya Jumia Deals.co.tz bila ya kujisajili. Lakini inapendekezwa sana ujisajili ili kuweza kupata faida zote za tovuti hii.
Ninatafutaje kitu flani kwenye tovuti ya Jumia Deals.co.tz?
Ni rahisi tu – nenda Jumia Deals.co.tz kisha chagua sehemu unayoishi, kisha anza kutafuta bidhaa unayohitaji.
Jinsi inafanya kazi

Umiliki wa matangazo yako

Ninarushaje tangazo?
Unaweza kurusha tangazo kwa kubofya kwenye kitufe hichi Rusha Tangazo Bure . Jaza maelezo kuhusu tangazo lako na wewe mwenyewe, weka picha kisha bofya kwenye sehemu ya Tengeneza Tangazo.
Nina rekebishaje tangazo langu?
Kurekebisha tangazo, bofya kwenye link ambayo umetumiwa kupitia barua pepe pale uliporusha tangazo lako. Au ingia kwa kutumia anuwani ya barua pepe na neno lako la siri kwa kubofya kwenye Akaunti Yangu . Tunakagua kila pale kitu kinabadilishwa. Ndio maana inaweza kuchukua muda wa dakika 30 mpaka uone mabadiliko yako kwenye tovuti.
Ninawekaje picha kwenye tangazo langu?
Kuweka picha kwenye tangazo lako, fuatahatua zile zile za kurekebisha tangazo lako. Weka picha kwa kubofya kwenye + kitufe kisha subiri wakati tangazo lako likikaguliwa.
Tangazo langu litaonekana kwenye tovuti kwa muda gani?
Tangazo lako litaonekana kwenye tovuti kwa muda wa siku 90. Ukiuza kifaa chako siku nyingi kabla ya muda huo, tunakuomba uondoe tangazo lako. Kama hujafanikiwa kuliuza, utapewa fursa ya kurusha tangazo lako upya likisha pitwa na wakati.
Kwanini ni ondoe tangazo langu?
Unaweza kuondoa tangazo lako ukishauza kifaa chako au ukiamua kwamba hutaki liuzwe tena. Kufanya hivi, tafadhali ingia kwenye tangazo lako kisha bofya kwenye kitufe cha Ondoa Tangazo ingiza neno lako la siri kisha chagua sababu ambayo imekufanya uondoe tangazo lako. Kisha bofya kwenye Ondoa Tangazo.
Ninawezaje kurusha tangazo langu kwenye mitandao ya kijamii?
Unaweza kurusha tangazo lako kwenye Facebook, Twitter, Pinterest na vinginevyo. Nenda kwenye tangazo lako kisha tafuta kitufe cha mtandao wa kijamii ambalo ungependa kulirusha, kisha bofya kwenye chaguo lako, au kwa njia tofauti unaweza kukopi na kunakiri linki ya tangazo lako na kuweka kwenye page unayohitaji.

Akaunti & Usajili

Ninasajili vipi akaunti yangu?
Ukisajili akaunti yako kwenye tovuti ya Jumia Deals.co.tz, akaunti yako ya kibinafsi itakuwa imetengenezwa. Akaunti yako itakuwezesha upange matangazo yako yote kwa njia moja na namba ya siri moja tu. Hii inamaanisha kwamba utaweza kurekebisha, kuondoa, na kupanga matangazo yako yote kwa urahisi.
Ninasimamia vipi matangazo yangu?
Kusimamia matangazo yako, ingia kwenye akaunti yako kwa kubofya kwenye kitufe cha Akaunti Yangu juu ya ukurasa. Muonekano wa matangazo yako utaonekana na utaweza kuchagua tangazo lako lipi ambalo ungependa kulisimamia kwa muda huo.
Je inabidi nijisajili kutumia Jumia Deals.co.tz?
Unaweza kukagua na kurusha matangazo yako kwenye tovuti ya Jumia Deals.co.tz bila ya kujisajili. Lakini inapendekezwa sana ujisajili ili kuweza kupata faida zote za tovuti hii.