SULUHISHO LA MATATIZO YA MOYO

SULUHISHO LA MATATIZO YA MOYO  - Tanzania
  • SULUHISHO LA MATATIZO YA MOYO  - Tanzania
Description :

Magonjwa ya Moyo ni magonjwa yanayoambatana na kuathiri moyo. Mara nyingi magonjwa ya moyo yanaambatana na mishipa ya damu kuwa na tatizo ambapo moyo hushindwa kufanya kazi, moyo hutegemea damu ambayo hubeba oxygen, madini, vitamins, kinga ya mwili, joto, homoni na vingine vingi.

Kwa mwaka 2015 pekee zaidi ya watu milioni 17.7 walifariki kutokana na magonjwa ya moyo na mfumo wa damu. Hii ni sawa na theluthi ya vifo vyote duniani. Zaidi ya theluthi ya vifo vyote vinavyotokana na ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu hutokea ndani ya nchi zenye uchumi wa chini na uchumi wa kati


Different-Problems-of-the-Heart.
AINA ZA MAGONJWA YA MOYO

Zipo aina mbalimbali za magonjwa ya moyo hutofautiana japo yote huathiri moyo, nayo ni;

Ugonjwa wa moyo unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu (Coronary artery disease) Hili ni tatizo linalowakuta watu wengi, mishipa ya damu hupasuka na kuharibika hii hutokana na mishipa ya damu kuwa na uchafu na mafuta mengi na kufanya damu isipite vizuri
Mapigo ya moyo kwenda tofauti (Heart Arrhythmias) Hii hutokea pale mapigo ya moyo kwenda taratibu isivyo kawaida au kwenda haraka isivyo kawaisda, pia mapigo ya moyo kwenda ovyo. Hii ni hatari sana na huua sana
Moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure) Hii ni hali moyo hushindwa kufanya kazi yake kama kupampu na kusambaza damu, kusambaza oxygen. Hii inaweza kutokea kwa mtu mwenye magonjwa kama ugonjwa wa moyo wa misipa kuathirika, Shinikizo la damu, na magonjwa mengine
Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa (Congenital heart disease) Haya ni magonjwa ambayo wengi huzaliwa nayo, yanaweza kuwa ni baadhi ya kasoro katika mwili kama baadhi ya chemba za moyo kuziba au kupasuka, oxygen kupita kwa shida na vinginevyo.
Ugonjwa wa valvu na misuli ya moyo (Heart Valve Disease & Cardiomyopathy (Heart Muscle Disease)) Katika moyo kuna chema nne nazo zinapitisha damu na oxygen kutoka kwenye mapafu, valvu hufunguka na kufunga. Valvu na misuli ikiwa imepasuka na kuharibika husababisha tatizo la moyo.
Moyo kutanuka. Hii hutokea pale damu ikiingia ndani ya moyo harafu mishipa ya kutoa damu ikiwa na tatizo ikashindwa kutoa damu nje ya moyo moyo utaanza kutanuka siku hadi siku. Kutanuka kwa moyo kunatokea usipotibu baadhi ya matatizo kama shinikizo la damu, moyo kwenda mbio, valvu na misuli ya moyo n.k.
Shinikizo la damu (B.P) ni shinikizo la damu yako kwenye kuta za mishipa yako kwani moyo wako unasukuma karibu na mwili wako. Unaweza kuwa na shinikizo la damu (shinikizo la damu) kwa miaka bila dalili yoyote.
Mshtuko/ Shambulio la moyo (Heart Attack). Ni kifo cha sehemu ya misuli ya moyo inayosababishwa na kuzuiwa wa usambazaji wa damu. Amana zilizo na mafuta huunda kwa wakati, na kutengeneza alama katika mishipa ya moyo wakoIkiwa baadhi ya misuli ya moyo inakufa, mtu hupata maumivu ya kifua na kukosekana kwa umeme kwa tishu za misuli ya moyo.
Chembe ya Moyo. Hii ni maumivu ya upande wa moyo maeneo ya kifua hutokea wakati unafanya kazi au hata kama umekaa kama ni yenye kukubuhu. Maumivu haya huambatana na kutokwa jasho na kukosa hewa. Hutokana na moyo kukosa damu ya kutosha.
CHANZO CHA MAGONJWA YA MOYO

Magonjwa ya moyo hutokea pale ambapo moyo huathiriwa na kuharibiwa kwa vitenda kazi vyake. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata magonjwa ya moyo nayo ni pamoja na;


Heart-Disease
Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P)
Kuvuta sigala
Uzito kupita kiasi na unene uliozidi
Kisukari
Kukaa sehemu kwa mda mrefu bila kuufanyisha kazi mwili
Umri
Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
Historia magonjwa yanayoambatana na moyo katika familia
DALILI ZA UGONJWA WA MOYO

Mara nyingi dalili hujionesha wakati mtu kakaa na ugonjwa kwa mda mrefu kidogo, ila kuna zingine zina
Moyo kwenda mbio (Moyo kudunda kwa nguvu isivyo kawaida )
Uchovu uliopitiliza, mwili kuwa d

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data