SIRI NA MAANA YA MAJIMAJI YA UKENI HII HAPA.

SIRI NA MAANA YA MAJIMAJI YA UKENI HII HAPA. - Tanzania
  • SIRI NA MAANA YA MAJIMAJI YA UKENI HII HAPA. - Tanzania
Description :

Uke wako hutoa maji maji ya aina gani?


Majimaji yanayotoka kwenye uke ikiwemo damu ya hedhi kitaalamu yanajulikana kama vaginal discharge yanaweza kuwa na rangi mbalimbali unaweza pia kujiuliza labda utakuwa unaumwa, kwani muda mwingine unaweza kuona yanatoka yakiwa na rangi ya tofauti kabisa. Kama ulivyo mkojo hubadili rangi hali kadhalika hata majimaji yanayotoka ukeni huweza kubadilika. Makala hii itakwenda kukueleza maana za kiafya kutokana na rangi za majimaji haya:-

Majimaji haya yana umuhimu mkubwa sana katika kulinda afya ya mwanamke na ujauzito. Miongoni mwa kazi zake ni:-
1.kuondoa uchafu mwilini mwa mwanamke

2.Kuondoa seli zilizokufa mwilini

3.Kulinda mimba dhidi ya bakteria, fangasi na virusi (kwa wajawazito)

4.Kulinda mwili wa mwanamke dhidi y ha vimelea vya maradhi visiingie kwenye mfumo wa kizazi kupitia ukeni

5. Kuweka mfumo wa kizazi katika usalama na ubora wake.

Kiasi cha majimaji yanayotoka ukeni huweza kutofautiana kwa rangi kulingana na siku katika mzunguruko wake wa hedhi
Kutokana na mizunguko kuwa tofauti kati ya mwanamke na mwanamke hivyo nitazungumzia kwa mifano kwa wenye mzunguko wa siku 28.

Kwa mfano:-

1. Siku ya 1 - 5 hapa ni mwanzo wa hedhi, kwa mwanake aliye katika umri wa kupata hedhi,,,,, majimaji yanayotoka kwenye uke wake yatakuwa ni mekundu ama yenye damu.

2.Siku ya 6 - 14 hii ni baada ya kukata kwa hedhi, hapa mwanamke hataona majimaji mengi kwenye uke kwake. Ila kadiri siku zinavyoenda yataanza kubadilika na kuwa kama mawingu ama rangi nyeupe pia yanaweza kuwa na rangi ya njano na kunatanata.

3. Siku ya 14 hadi 16 hapa yai linakuwa limesha toka, hivyo majimaji yanaanza kuwa na utelezi mwingi na kufanana na yale majimaji meupe ya yai baada ya kulivunja hii ndo tunaita ute wa uzazi. Siku ya 17-25 yanarudi kuwa na mawingu, meupe ama njano.

4. Siku ya 25 - 28 majimaji haya yatakuwa mepesi sana na ni machache sana, mzunguko unakuwa umeisha tunaanza upya tena

Ok tumeshaona mabadiliko hayo ya majimaji yanavyobadilika kulingana na siku. Sasa hebu tuone badiliko la hizi rangi zinatuambia nini kiafya:-

1.rangi nyekundu:-
Hii ni damu ya hedhi, mara nyingi damu hii inakuwa ni anga’vu na yenye kufanana na rangi ya kutu. Hii ni kawaida kwa wanawake wote hivyo inaashiria afya ya kawaida. Na endapo itatoka kwa siku nyingi zaidi ya wiki, kiafya haionyeshi usalama (mvurugiko wa homoni au shida ya uvimbe kwenye KIZAZI n.k). Ni vyema kumuona daktari aliye karibu nawe.

2. rangi nyeupe

Majimaji meupe yanaweza kuwa na rangi kama ya cream ama njano iliyo pauka. Kama mwanamke hana dalili zozote basi rangi hii inaonyesha mwanamke huyo yupo katika afya njema.

Hata hivyo ikiwa majimaji haya ni meupe na yameshikamana kama maziwa ya mgando au yakiwa yana harufu kali inaweza kuashiria kuna maambukizi ya vimelea vya maradhi kama fangasi na bakteria.

Ila kwa mara nyingi majimaji meupe yakiwa mazito, yana harufu kali hali hii inahusiana na maambukizi ya fangasi.
Hali hii inaweza kusababisha miwasho katika baadhi ya nyakati au muda wote.

3. Rangi ya njano kuelekea ukijani
Kama majimaji haya yana rangi ya njano huenda hakuna tatizo ila yakiwa ni njano iliyowiva ama njano iliyo na ukijani ama majimaji haya yakiwa ni ya kijani hii huashiria maambukizi ya bakteria ama magonjwa ya zinaa, fika kituo cha afya kama yatakuwa yanatoa harufu mbaya.

4. rangi ya kahawia

Majimaji ya rangi hii yanakuwa na damu kwa mbali. Hali hii ni kawaida kama itatokea siku chache kabla ya kuingia hedhi. Pia inaweza kuashiria mimba changa. Na majimaji haya yatakuwa yanatokea baada ya kukutana kimwili, hii inaashiria kuwa kuna michubuko imetokea kwenye uke na kusababisha mipasuko midogo iliyokuwa ikivuja damu..

5. majimaji yaliyo safi meupe
Katika hali ya kawaida majimaji yanayotoka ukeni yana kuwa ni safi na yenye weupe na yenye kuteleza kama vile majimaji meupe yanayotoka baada ya kupasuka yai.

6. rangi ya kijivu
Majimaji ya rangi ya kijivu sio ya kawaida hivyo yanaashiria hali mbaya kiafya hivyo muone daktari au tucheki .

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data