KUTOSHIKA MIMBA NA TIBA YAKE.

KUTOSHIKA MIMBA NA TIBA YAKE. - Tanzania
  • KUTOSHIKA MIMBA NA TIBA YAKE. - Tanzania
Description :


Tatizo la kutopata mimba linawasumbua wengi na huwapata familia kadhaa katika jamii, huweza kumpata mtu mmoja kati ya wanandoa 12 na ni tatizo linalowapata watu zaidi ya milioni 24 duniani kote.

Ugumba ni hali ya kutoweza kupata ujauzito katika kipindi cha mwaka mmoja au zaidi kwa wenzi ambao wamekuwa wakifanya mapenzi bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango. Mtiririko wa upataji ujauzito ni kama ifuatavyo;

Baada ya mwezi mmoja wa ndoa uwezo wa kushika ujauzito ni asilimia 20, baada ya miezi mitatu ya ndoa ni asilimia 50, baada ya miezi sita ya ndoa ni asilimia 75 na baada ya miezi 12 ni asilimia 90 mwanamke huweza kupata ujauzito.

Hali hii inaweza kutokea kutokana na tatizo kwa mwanaume au mwanamke, ingawa baadhi ya watu wamekuwa wakidhani wanawake peke yao ndio ambao hupata tatizo hilo.

Tatizo hili limegawanywa katika vipengele viwili kimoja ni kile ambacho mwanamke hushindwa kupata mimba baada ya mwaka mmoja wa kufanya tendo la ndoa na mume wake bila kutumia kinga kwa mwanamke mwenye umri chini ya miaka 35 (primary infertility).

Kipengele cha pili ni kile kijulikanacho kama 'secondary infertility' ambapo mwanamke hushindwa kubeba mimba wakati siku za nyuma alishawahi kupata ujauzito.

Tatizo la ugumba huweza kupatiwa matibabu na kuisha.

KUNA TAFAUTI GANI KATI YA UGUMBA NA UTASA?

Tofauti na ugumba, utasa ni hali ya mwanamke kutoweza kushika ujauzito kabisa au mwanaume kutoweza kusababisha ujauzito kwa mwanamke kabisa.

Mtu tasa hana uwezo wa kupata mimba au kumpa mwenzi wake mimba kabisa, wakati mgumba ana uwezo wa kuja kupata mimba iwapo tatizo litaondolewa.

NINI HUSABABISHA UGUMBA?

Kuna sababu mbalimbali ambazo hupelekea ugumba kutokea kwa mwanaume au mwanamke.

WANAUME
Ugumba kwa wanaume hutokana na tatizo katika mbegu za kiume, manii kuwa kidogo, manii kushindwa kutembea, manii kuwa na umbo lisislo la kawaida au kuziba kwa mijira ya mbegu za kiume.

Tatizo kwenye mbegu za kiume linaweza kutokana na;

- Uvutaji wa sigara
- Dawa za kulevya kama matumizi ya bangi kwa wingi,
- Mionzi (radiations)
- Unywaji wa pombe
- Kemikali kama DDT, risasi (lead)
- Kufanya kazi mazingira yenye joto kali kama viwanda vya chuma.
- Kuziba kwa mirija ya mbegu za kiume kutokana na magonjwa ya zinaa

WANAWAKE
Tatizo la ugumba husababishwa na sababu kuu mbili:

- Kuziba kwa mijrija ya kupitisha mayai
- Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi au kutoa mayai isiokuwa na nguvu (lazy egg).

Mirija ya kupitisha mayai inaweza kuziba kutokana na;

- Ugonjwa wa Pelvic Inflammatory Disease (PID) ambao unatokana na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa kama kisonono na klamidia.
- Mirija ya mayai kujaa maji
- Utoaji mimba usio salama (unsafe abortions)
- Upasuaji maeneo ya kiunoni
- Ugonjwa wa endometriosis

Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi inaweza kutokana na;

- Umri mkubwa wa mwanamke, hasa miaka 35 – 40 na kuendelea.
- Uvutaji wa sigara
- Saratani ya Ovari
- Mionzi (radiations)
- Ugonjwa wa Polycystic ovarian disease (Ovarian Cyst)

Sababu nyingine za ugumba kwa mwanamke zinaweza kuwa;

- Makovu katika mji wa uzazi kutokana na kutoa mimba.
- Mabonge ya kizazi (uterine fibroids)
- Kuziba kwa shingo ya uzazi
- Kulegea shingo ya uzazi
- Kisukari
- Matatizo ya tezi ya shingo (hyperthyroidism)
- Kufanya mazoezi ya kupitiliza (excessive exercising)

VIPIMO VYA KUJUA UGUMBA

Vipimo mbalimbali vinapatikana ili kuwezesha kugundua chanzo cha ugumba. Licha ya uwezo wa vipimo hivi, zaidi ya asilimia 10 ya watu wenye tatizo hili chanzo kinaweza kisijulikane kabisa. Ni vizuri kwa wenzi wote wawili wenye tatizo hili kuonana na daktari kwa ajili ya ushauri na vipimo.

KWA WANAUME HUFANYIKA;

Kipimo cha manii (seminalysis) kuona kama manii zipo za kawaida na kwa kiwango kinachoatakiwa. Manii huchukuliwa kwa kondomu maalum wakati wa kufanya mapenzi au kwa kupiga punyeto na kisha kuchunguzwa kwa darubini.
Kwa Msaada Zaidi Wasiliana Nasi.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data