KUTOKWA NA UCHAFU UKENI NA TIBA YAKE

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI NA TIBA YAKE - Tanzania
  • KUTOKWA NA UCHAFU UKENI NA TIBA YAKE - Tanzania
Description :

Aina Za Uchafu Wa Ukeni Usio Wa Kawaida


Kitu cho chote kitakachoharibu uwiano wa bakteria wa kawaida waishio katika uke kinaweza kuleta mabadiliko katika rangi, harufu au muundo wa uchafu utakaotoka katika uke. Hapa chini naonyesha aina ya uchafu unaotoka, maana yake au chazo chake na dalili ambazo zitatokea kwenye mwili wa mwanamke husika:

Uchafu Wenye Damu Au Wa Rangi Ya Kahawia

Hii ni dalili ya mzungumko wa mwezi wa mwanamke uliovurugika na mara chache ni dalili ya kansa ya Cervix au aina nyingine ya kansa iitwayo endometrial cancer. Mwanamke mwenye tatizo hili atatoa damu nyingi ukeni na kuumwa nyonga.

Uchafu Wenye Rangi Ya Mawingu Au Njano

Hii ni dalili ya ugonjwa wa kisonono (Gonorrhea). Mwanamke atatokwa na damu katikati ya siku zake, atatokwa na mkojo bila kukusudia na kupata maumivu ya nyonga.

Uchafu Wa Njano Au Kijani Wenye Harufu Mbaya,
Endapo uchafu utatoka kama mapovu, wenye rangi ya kijani au njano ukiambatana na harufu mbaya , hii ni dalili ya Trichomoniasis, maambukizi (parasitic) yanayotokana na ngono zembe. Dalili nyigine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo.

Uchafu Mweupe Mzito Kama Jibini

Hii ni dalili ya maambukizi ya aina ya fungus (Yeast infection) na dalili nyingine atakazozisikia mwanamke huyu ni kuvimba na maumivu kwenye sehemu za nje za siri (vulva), kuwashwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Uchafu Mweupe, Wa Njano Au Wa Kijivu Wenye Harufu Ya Samaki

Uchafu wa aina hii ni dalili za maabukizi ya Bacterial Vaginosis. Mwanamke mwenye tatizo hili atasikia miwasho au maumivu, kuvimba kwa uke au sehemu ya nje ya uke (vulva).

Aina Ya Maambukizi Ya Ukeni
Kuifanya mada yetu iwe na maana na msaada zaidi, tutazungumzia kwa undani zaidi aina chache za maambukizi ya ukeni ambazo zinawasumbua wanawake wengi zaidi, ambapo tutatazama dalili zake na kuelezea tiba ambazo zinawea kutolewa kuondoa matatizo hayo. Hapa tutazungumzia Bacterial Vaginosis, Trichomoniasis na Monilia (Yeast) Infection.

Bacterial Vaginosis: Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakifahamiki. Kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya bacteria hawa ambao ni kawaida kupatikana kwenye uke na kubadilisha uwiano wao kwenye mazingira ya uke. Wanawake wenye wapenzi wengi au wanaofanya mapenzi kupitia midomo wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ya Bacterial Vaginosis.

Dalili za Bacterial Vaginosis:

– Kuongezeka kwa uchafu unaotoka ukeni

– Kutokwa na uchafu wa kijivu/mweupe, mwepesi au wa majimaji

– Harufu kama ya samaki ikiambatana na uchafu

– Harufu inayozidi au uchafu unaozidi mara baada ya kufanya tendo la ndoa

Tiba kwa tatizo la bacterial vaginosis zipo za aina mbili. Tiba ya aina ya kwanza ni kutumia metronidazole (Flagyl) na tiba ya pili ni kutumia antibiotic ya vidonge au ya cream.

Trichomoniasis: Maambukizi haya hutokana na aina ya protozoa wa seli moja. Trichomoniasis maranyingi huambukizwa kwa kufanya ngono. Protozoa huyu huweza kukaa kwenye mazingira ya unyevunyevu kwa muda wa saa 24 bila kufa hivyo kufanya taulo na nguo nyingine za kuogea kuwa chanzo kingine kikuu cha maambukizi.

Dalili Za Trichomoniasis
– Kutokwa na uchafu wa rangi ya njano/kijani ulio kama mapovu
– Harufu mbaya inayoambatana na kutokwa na uchafu
– Kuongezeka kwa uwingi wa uchafu wa ukeni
– Maumivu ya ukeni au sehemu za nje ya uke (vulva)
– Kujisaidia haja ndogo mara nyingi zaidi
– Kuwashwa sehemu za siri.

Monilia (Yeast) Infection: Kwa kawaida kuna kiwango kidogo cha yeast (Candida albicans) katik uke. Tunasema kuna maambukizi ya yeast pale kiwango chao kinapozidi hali ambayo inatokana na kubadilika kwa hali ya ukeni (change in the pH balance of the vagina). Maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la ngono. Kuna mambo ambayo yanaweza kusababisha kuongezeka kwa yeast katika uke, nayo ni; msongo wa mawazo, matumizi ya dawa za kuziua mimba, kisukari, ujauzito.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data