KUTOKWA NA DAMU WAKATI WA HAJA KUBWA

KUTOKWA NA DAMU WAKATI WA HAJA KUBWA - Tanzania
  • KUTOKWA NA DAMU WAKATI WA HAJA KUBWA - Tanzania
Description :

Angalizo (Siyo Kila Unapoona Kuna Damu Inavuja Ni Bawasili)

Unapoona kuna damu inavuja mahala pa haja kubwa ama unapotoa haja, nashauri nenda haraka hospital kuonana na Dactari na kufanya vipimo.
Hasa kama tatizo ni limekutokea kwa mara ya kwanza.
Kuvuja kwa damu kwenye sehemu ya haja kubwa inaweza kuwa ni dalili za Saratani ya utumbo mpana .

Kitu kimoja cha kuvutia sana ni kwamba uwepo wa Vitamn D ya kutosha mwili hupunguza hatari ya kupata bawasili kwa karibu 80%. Kwahiyo kama tatizo linajirudia mara kwa mara basi fanya checkup kujua kama una vitamn D ya kutosha.


Vihatarishi/ Visababishi Vingine Vya Tatizo La Bawasiri

Kufanya mapenzi kinyume na maumbile

Kuharisha kwa muda mrefu
Kukaa kitako kwa muda mrefu
Matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu
Dalili zingine za zitakazokusaidia kugundua kama una tatizo la bawasili ni;

Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
Kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
Kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
Kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
Hatua Nne Za Kuzuia Kutokea Kwa Bawasiri
Hapo juu tumeona kwamba chanzo kikubwa cha tatizo hili ni matatizo ya mfumo wa umen’genyaji kama kukosa choo kwa mda mrefu, kupata choo kigumu, kuharisha mara kwa mara na tumbo kujaa gesi, hivo kwa kuzuia matatizo haya basi utakuwa umejikinga na bawasili. Hivo hakikisha unafanya yafuatayo;

Kula mbogamboga za majani, na nafaka zisizokobolewa, matumizi ya vyakula vya nyuzinyuzi kwa wingi husaidia kuongeza ukubwa wa kinyesi na hivo kurahisha utolewaji wake, kama mwanzo hukutumia vyakula vya nyuzinyuzi basi anza kuongeza taratibu kwenye mlo wako mpaka pale tumbo litakapozoea.

Tumia machungwa kwa wingi, machungwa yana kiungo kinachoitwa flavonoids, kiungo hiki ni muhimu katika ustawi wa mishipa ya damu ya Veins, mishipa hii ndio huathirika na kuletekeza bawasiri.
Kunywa maji ya kutosha kila siku, tumia kiu na rangi ya mkojo kama kiashiria cha kiasi gani cha maji unatakiwa kunywa, kama mkojo ni wa rangi ya njano inayokolea basi ni kiashiria kwamba mwili hauna maji ya kutosha na unatakiwa kunywa. Nyuzinyuzi na maji ya kutosha husaidia kulainisha choo chako na hivo kurahisisha utolewaji wake bila kujikamua.
Hakikisha unapata virutubisho kwa ajili ya kusawazisha bacteria wazuri ndani ya mfumo wa chakula, vyenye ubora wa hali ya juu usimeze kila kirutubisho.Kama huna chanzo kizuri cha kupata virutubisho hivi tunashauri fika ofsini kwetu kupata usaidizi.
Zingatia haya Ukiwa Chooni

Ruhusu mwili wako kufanya kazi kwa jinsi ulivoumbiwa, yaani pale unapojiskia haja basi hakikisha unaenda mara moja kujisaidia pasipo kujizuia, kujichelewesha kunaweza kusababisha Constipation.

Usikae mda mrefu chooni ukijisaidia, hii inaongeza mgandamizo katika eneo la chini kwenye mishipa ya damu na hivo kukuongeza hatari ya kupata bawasili.

Tumia dakika 3 mpaka 5, ama subiri mpaka unapokuwa na haja, kama unajiskia kutoa uchafu lakni ukienda chooni kinyesi hakitoki basi tembea tembea ama fanya zoezi la Squats.

Usitumie nguvu kubwa kujikamua kutoa haja, tumia misuli ya tumbo kutoa haja taratibu.
Unapotoa haja basi hakikisha unachuchumaa kama miili yetu ilivoumbwa. Watu wanaotumia njia hii mara chache sana huugua bawasili, lakini matumizi ya vyoo vya kukaa ni moja ya kihatarishi cha kupata bawasili kutokana na kwamba inahitajika utumie nguvu kubwa sana kujikamua.

Tumi njia salama Kujisafisha
Usitumie nguvu kubwa kujifuta kwa toilet paper ama wipes zingine baada ya kwenda haja, hii hufanya ngozi kulanika na kuvimba
Kama inawezekana jisafishe taratibu kwa kutumia maji bila sabuni, na kujifuta kwa taulo laini.

Kwa maeneo ambapo huwezi kutumia maji mfano kwenye vyoo vya umma, basi tumia wipes laini zenye unyevunyevu kwa umakini.

Kama teali ni muhanga wa changamoto karibu upate matibabu wasiliana nami apo chini.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data