KUTOKA UCHAFU UKENI WENYE HARUFU

KUTOKA UCHAFU UKENI WENYE HARUFU - Tanzania
  • KUTOKA UCHAFU UKENI WENYE HARUFU - Tanzania
Description :

Utunzaji wa Uke na Usafi
Kutunza uke na kulinda afya ya uke ni jambo la muhimu sana kwa mwanamke. Kutokwa na harufu mbaya ukeni ni kiashiria kwamba unaumwa na hauko sawa. Hali hii inaweza kuathiri heshima ya mwanamke na pia mahusiano na mwenza wake.

Harufu mbaya ukeni kwa kiasi kikubwa husababishwa na fangasi wa candida. Japo siyo kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke.

Kama wewe muhanga wa tatizo hili basi tambua kwamba kuna njia za asili unaweza kuzitumia ikiwemo lishe na virutubisho na ukarudi katika hali ya kawaida. Kesi chache sana kama tatizo litazidi kuendelea basi itatakiwa uende hospitali ili upate uchunguzi.

Ni kawaida kwa mwanamke kupata harufu ukeni kutokana na hali ya uke kujisafisha kutoa vimelea wabaya. Lakini pale harufu inapokuwa kali sana mfano wa harufu ya shombo la samaki basi ujue kuna tatizo kubwa. Kutokwa na harufu mbaya ukeni huwa inaambatana na dalili zingine kama kuwasha na kuchomachoma na kutokwa na majimaji.

Nini Kinasababisha Harufu Mbaya Ukeni
Ukuaji wa Bacteria (Bacteria vaginosis)
Sababu namba moja ya kupata harufu mbaya ukeni ni ukuaji wa bacteria. Bacteria Vaginosis ni ukuaji wa bacteria usio wa kawaida kwenye uke. Rejea maelezo ya pale juu kuhusu sababu ya kukua kwa bacteria wabaya kwenye uke ikiwa ni pamoja na kubadilika kwa mazingira ya ukeni na kushuka kwa kinga.

Bacteria vaginosis inaweza kupelekea mimba kuharibika, kujifungua kabla ya wakati na kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa mengine ya ngono. Dalili mojawapo ya kwamba tayari una maambukizi ya bacteria ni kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu kali mfano wa harufu ya samaki wabichi

Trichomoniasis
Trichomoniasis ni moja ya ugonjwa wa ngono unaosababisha harufu kali ukeni. Ugonjwa huu husababishwa vimelea na huambatana na kutokwa na uchafu ukeni,kuwasha, na maumivu makali wakati wa kukojoa.

Trichomoniasis inaweza kuwaathiri wajawazito na kuleta hatari ya mimba kutoka. Kama utagundua una Trichomoniasis basi wewe na mwenza wako mnatakiwa kutibiwa. Hakikisha pia unatumia condom vizuri kila unapofanya ngono kama kinga dhidi ya magonjwa haya.

Mabadiliko ya Homoni
Mabadiliko ya homoni kutokana na mzunguko wa hedhi unaweza kuchangia harufu mbaya ukeni. Wanawake wanaokaribia kukoma hedhi wapo kwenye hatari zaidi kwani homoni ya estrogen hupungua sana na hivo kusababisha tishu za kuwa na tindikali kidogo.

Kutozingatia Usafi na Kutokwa sana na Jasho
Ni wazi kwamba uchafu na kuwepo kwa unyevunyevu sehemu za siri huzalisha harufu mbaya. Kisayansi ni kwamba tezi zilizopo ndani ya mwili (apocrine sweat glands )hutengeneza mafuta kuelekea kwenye maeneo ya mwili.

Maeneo haya ni kama kwapa, pua, ndani ya sikio, uke, na kwenye chuchu. Bacteria waliopo maeneo hayo huchakata mafuta haya na hivo kuzalisha harufu kali. Uvaaji wa nguo zilizobana na uzito kupita kiasi huchangia kuhifadhiwa kwa jasho kwenye mikunjo ya ngozi na hivo kuletekeza harufu.

Kuvaa Pedi kwa Masaa Mengi
Pedi inapovaliwa kwa muda mrefu husababisha ngozi kucharuka,kututumka na kuwasha na pia. Hali hii huchangia kukua kwa bacteria na fangasi wabaya ambao ni chanzo cha harufu.

Hatua 6 za Kujikinga dhidi ya Harufu Mbaya Ukeni
1.Vaa nguo za ndani za pamba, zisizobana sana.
Nguo zilizoabana zinazuia kupita kwahewa safi kuelekea ukeni na hivo kusababisha unyevunyevu ambao ni mbolea kwa bacteria na fangasi wanaoleta harufu mbaya kwenye uke. Hakikisha unabadilisha chupi kila baada ya masaa 12 inasaidia kuzuia kukua kwa bacteria wabaya.

2.Badili Nguzo zako Kila Baada ya Kufanya Mazoezi
Nguo zenye unyevu ni mbolea nzuri kwa ukuaji wa bacteria hivo hakikisha unavaa nguo zilizokauka na kubadilisha kila baada ya kutoka mazoezini.

3.Punguza uzito kama inawezekana
Uzito mkubwa na kitambi vinakufanya utokwe na jasho kwa wingi zaidi hasa kwenye uke. Na kama tulivojifunza pale juu, jasho na unyevunyevu inaleta fangasi na bacteria wabaya. Chagua kula lishe nzuri na kufanya mazoezi ili kurekebisha mwili wako. Karibu pate huduma kama unaswali ulizi

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data