Jitibu PID,fungus na miwasho ukeni

Jitibu PID,fungus na miwasho ukeni - Tanzania
  • Jitibu PID,fungus na miwasho ukeni - Tanzania
Description :

Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.PID husababishwa na nini?

Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.

Je mwanamke huambukizwaje PID?

Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na
Kufanya ngono isiyo salama
Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango, na
Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.


Dalili za PID ni zipi?
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni
Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
Kupata maumivu ya mgongo
Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
Kupata homa
Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na
Pia kutapika

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data