Jinsi Ninavyo Wasaidia Wanawake Wenye Kutokwa Na Uchafu Sehemu Za Siri Bila Chemical Yoyote

Jinsi Ninavyo Wasaidia Wanawake Wenye Kutokwa Na Uchafu Sehemu Za Siri Bila Chemical Yoyote - Tanzania
  • Jinsi Ninavyo Wasaidia Wanawake Wenye Kutokwa Na Uchafu Sehemu Za Siri Bila Chemical Yoyote - Tanzania
Description :


Hello,Unajua kwanini mwanamke hutokea na uchafu sehemu za Siri pamoja na harufu Mbaya ?
hivyo nimekuandalia ujumbe muhimu ambao utakuwa msaada wako nimeonyesha jinsi ya kuondokana na tatizo hilo bila ya kuweka machemical mengi sasa. Kwanza tujue kutokuwa uchafu kwa mwanamke ni nn?

hii siyo hali ya kawaida mwanamke kutokwa na majimaji au uchafu ukeni au sehemu za siri.Tatizo hili hutamkwa ‘lukorea’ na huwapata zaidi wanawake walio katika umri wa kuzaa ingawa hata wasichana wadogo na wazee pia huwatokea lakini kwa idadi ndogo. Mwanamke kuwa na tatizo hili haihusiani na mfumo wa mkojo ingawa kumekuwepo na desturi ya wanawake wanapokuwa na hali hii isiyo ya kawaida huita kimakosa yutiai hivyo hujikuta wanapata tiba isiyo stahili.

chanzo cha tatizo

lukorea kama ilivyo siyo ugonjwa bali ni dalili ya magonjwa yaliyojificha kwa mwanamke katika viungo vyake vya uzazi ambapo ni ukeni na katika mlango wa kizazi na hata mwilini kwa ujumla kama ana magonjwa sugu ya mfumo wa mwili kifua kikuu, kisukari, kansa na upungufu wa kinga mwilini au hiv.

vijidudu vinavyosababisha maradhi haya ni aina ya bakteria, protozoa na fangasi. Visababishi vingine ni vijidudu aina ya parasaiti ambao hujificha ukeni, kuwepo na vitu visivyo vya kawaida ukeni, matatizo ya kizazi na nyonga, matatizo katika mfumo wa homoni, kusinyaa kwa uke hasa katika umri mkubwa, vidonda ukeni, kutokuwa msafi ukeni na kutokwa na ute mzito ukeni hasa kama unatumia baadhi ya dawa za homoni, mfano vidonge vya kuzuia mimba. Matatizo mengine yanayochangia ni tiba za mionzi mfano kwa wenye kansa ya shingo ya kizazi huweza kutokwa na majimaji ukeni pamoja na matumizi ya vipodozi ukeni.

pamoja na yote, magonjwa ya zinaa kutokana na vijidudu vya trikomonia na gono pia huchangia hali hii. matatizo mengi ya kutokwa na uchafu mzito ukeni husababishwa na fangasi aina ya candida au monilia, bakteria wakubwa wanaohusika ni aina ya gonococcal, spirochetal, staphylococcal, streptococcal, pneumococcal na tuberculosis, ambapo siyo sana.

aina za tatizo kutokwa na majimaji sehemu za siri kwa watoto

watoto wachanga na watoto wadogo ambao hawajavunja ungo wanaweza kupatwa na tatizo hili la kutokwa na hali kama ya majimaji ukeni na yakamshtua mzazi au mlezi. Hali hii siyo ya kawaida na huwa haitoki ukeni kwa ndani. Chanzo chake huwa katikati ya midomo ya uke au valvu, mara chache sana huanzia ukeni kwa ndani.

chanzo cha tatizo hili kwa watoto ni uchafu, minyoo au wakiingiliwa na vitu visivyo vya kawaida ukeni na endapo watasuguliwa sana sehemu zao za siri wakati wa kunawishwa au kuogeshwa. Kusuguliwa huku sana kwa watoto katika sehemu zao za siri huitwa masturbation na husababisha watoto wapate tatizo hili la kutokwa na majimaji kwa hiyo tuwe waangalifu tunapowasafisha watoto wa kike. Uchafu unaweza kusababishwa na kukaa na nepi yenye kinyesi au mkojo kwa muda mrefu bila ya kumbadilisha na kutomsafisha kwa maji baada ya kujisaidia haja kubwa.

vitu visivyo vya kawaida ni mchanga, kama mtoto hatavalishwa chupi na nguo salama anapocheza hivyo mchanga hujipenyeza katika sehemu zao za siri. Mtoto mwenye tatizo hili wakati mwingine utaona sehemu zake za siri zimevimba na nyekundu na muda wote analia tu maumivu hasa ukimgusa na unaweza kudhani ameingiliwa au amechezewa kumbe ni uzembe wako mzazi kutokuwa msafi.

tatizo kwa mabinti

hapa tunazungumzia kutokwa na majimaji au uchafu kwa mabinti ambao ni bikira, hao pia hutokewa na hali hii. chanzo ni kama kilekile au vilevile tulivyoviona kwa watoto. Ingawa baada ya kuvunja ungo hupatwa na hali ya kutokwa na majimaji yasiyo na maambukizi mara kwa mara au kila siku na kujihisi wanalowa.

hali hii hutokana na mfumo wao wa uzazi sehemu za ukeni ambapo hufanya sana kazi katika kipindi hiki cha mpito cha balehe. Kwa hiyo kama hakuna muwasho, harufu mbaya wala maumivu, huwa tunasema ni hali ya kawsida.
hivyo kwa ujumla nimeweza kutoa mafunzo bure kwa wanawake waliosumbuliwa na hali kama yako.Nahivyo kama utakuwa tayar naomba utoe comments hapo chini

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data