Je, BAWASIRI HUTIBIKA BILA UPASUAJI?

Je, BAWASIRI HUTIBIKA BILA UPASUAJI? - Tanzania
  • Je, BAWASIRI HUTIBIKA BILA UPASUAJI? - Tanzania
Description :

Jibu Ndio Bawasiri hutibika
BAWASIRI (HEMORRHOIDS)*

Ugonjwa wa Bawasiri (Hemorrhoids) husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
-Tatizo hilo huleta maumivu sana, mishipa ya damu (veins) inapovimba ndani ya mfereji wa haja kubwa na kusababisha bawasiri ya ndani na uvimbe huo unapoonekana kwa nje huitwa bawasiri ya nje,
pia yawezekana ukawa na aina zote za bawasiri kwa wakati mmoja.

*Kuna aina kuu mbili za bawasiri nazo ni :-*

1⃣Bawasiri ya nje
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Wakati mwingine mishipa ya damu (veins) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina nyingine ya bawasiri kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

2⃣Bawasiri ya ndani
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wana tatizo hili bali hujulikana kwa kuona kinyesi ulichotoa kimeambatana na damu, pia bawasiri ya ndani hutoka mpaka nje ya sehemu ya kutolea haja kubwa.

▪Aina hii imegawanyika katika aina zingine zifuatazo;-

▪Daraja I- Bawasiri kutoka katika mahali pake pa kawaida.
▪Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
▪Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
▪Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

*SABABU ZA BAWASIRI *

mishipa ya vein inayoizunguka sehemu ya haja kubwa huvutika kutokana na msukumo na hatimaye kuvimba. Mishipa iliyovimba (bawasiri) huweza kuendelea kukua sehemu ya kutolea haja kubwa, sababu zinazosababisha msukumo huo uongezeke ni pamoja na;

▪Msukumo mkubwa wakati wa kutoa haja kubwa
▪Kutumia muda mrefu chooni wakati wa kujisaidia haja kubwa
▪Kuharisha au tatizo la kukosa choo
▪Kuwa na uzito mkubwa
▪Mimba
▪Kumwingilia mwanamke sehemu ya haja kubwa
▪kutokula vyakula vya faiba
▪Kutokwa na choo kikubwa bila kutarajia.

*Dalili za Bawasiri*
Dalili na tiba hutegemea una aina gani ya bawasiri, nguvu nyingi inayotumika kwenye kiuno au sehemu ya mwisho ya utumbo mkubwa wakati wa kutoa haja kubwa huweza kusababisha bawasiri, mara nyingi tishu iliyo ndani ya sehemu ya kutolea haja kubwa huwa na damu ili kusaidia usafirishaji wa haja kubwa. Ikiwa utanyanyua vitu vizito au ukiwa chooni kwa muda mrefu wakati wa kujisaidia haja kubwa, shinikizo (pressure) iliyoongezeka husababisha mishipa ya damu kwenye nyama (tissue) ivimbe na kuvutika, hali hii husababisha bawasiri. dalili nyingine ni kama;

▪Kuharisha au kutopata choo kikubwa, hii pia huongeza shinikizo(pressure) katika mishipa ya damu ya vein katika mfereji wa haja kubwa.
Mama wajawazito wanaweza pata bawasiri wakati wa miezi 6 ya ujauzito, hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa shinikizo (pressure) kwenye mishipa ya damu ya kiunoni.pia wakati wa kusukuma motto kipindi cha kujifungua huweza kusababisha bawasiri.
Kuwa na uzito mkubwa pia husababisha bawasiri.
▪Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa.
▪Kuwashwa au kujikuna sehemu ya haja kubwa.
▪Kuvimba pembeni ya sehemu ya haja kubwa.
▪Kuhisi maumivu sehemu ya haja kubwa.
▪Kuwa na jipu sehemu ya haja kubwa na kuhisi maumuvu.

*Madhara yasababishwayo na Bawasiri*

✔Upungufu wa damu mwilini (Anemia), bawasiri huweza kusababisha seli nyekundu za damu zisisafirishe hewa ya oksijeni kwenye seli zako, na hali hii
✔husababisha uchovu.,

*NJIA ZA KUZUIA BAWASIRI *

✔ Kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi. Pia
✔Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita hadi nane kwa siku) ili kulainisha choo.
✔Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa wakati wa kutoa haja kubwa.
✔Punguza uzito wa mwili wako, kuwa na uzito mkubwa wa mwili kunaufanya upate bawasiri.
✔Jisaidie pale unapohisi haja.
TUMIA NOVEL NA CONSTRELAX Kujitibu. Wasiliana nasi kupata suluhu.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data