IJUE SABUBU YA PUMU KWA WATOTO NA NAMNA YA KUITIBU.

IJUE SABUBU YA PUMU KWA WATOTO NA NAMNA YA KUITIBU. - Tanzania
  • IJUE SABUBU YA PUMU KWA WATOTO NA NAMNA YA KUITIBU. - Tanzania
Description :


Nini maana ya Pumu?
Pumu ni hali ambayo huathiri njia za hewa, njia hizi za hewa pia huitwa mirija ya kupumulia. Mirija hii huanzia kwenye njia ya hewa(trachea) hadi kwenye mapafu.

Mchakato wa kupumua kwa watoto walio wengi ni rahisi : Watoto huingiza hewa kupitia puani au mdomoni na hewa huingia kwenye njia ya hewa(trachea) na kuelekea kwenye mapafu. Lakini Kwa watoto wenye pumu, hupumua Kwa shida Kwa sababu njia ya hewa hushindwa kupitisha hewa kwa sababu ya njia yao kuwa imehathiriwa na hali ya pumu.

Shambulio la pumu (Asthma attack) ni nini?
Hii ni hali ambayo hutokea wakati njia ya hewa inapo vimba na kuwa nyembamba na inakuwa vigumu kwa hewa kuingia na kutoka kwenye mapafu. Wakati mwingine njia za hewa zinapokuwa zimevimba hutoa majimaji mfano wa makamasi, hali ambayo husababisha mchakato mzima wa mabadlishano ya hewa katika mapafu kuwa mgumu na hii hali ndo inapelekea tatizo zima la mtotoanapo patwa na pumu kushindwa kupumua vizuri.

Wakati ugonjwa huu unaanza, upumuaji kwa mtoto unaweza kuwa wa kawaida na kuonekana kama vile hakuna tatizo, Lakini kipindi ugonjwa unapoanza, unaweza kuhisi kwamba mtu anapumua kupitia kwenye mrija. Mtoto mwenye pumu anaweza kutoa mlio kama wa filimbi (anapopumua), kukohoa, na kusikia kifua kubana.

Wakati shambulio la ugonjwa wa pumu(asthma attack), hali inaweza kuwa mbaya zaidi kama mtoto hatatumia dawa sahii za pumu. Baada ya kutumia dawa na kupata matibau sahii wakati wa shambulio la ugonjwa wa pumu, njia ya hewa mara nyingi hurudia hali yake ya kawaida, ingawa inaweza kuchukua muda mrefu kidogo wakati mwingine.

Pumu huwapata watu gani?
Pumu ni ugonjwa ambao huwapata watu wengi zaidi ya unavyo weza kufikiri.Karibia watoto milioni sita nchini marekani wanaumwa ugonjwa wa pumu(Hatujui hapa kwetu Tanzania ni idadi gani?).Ugonjwa wa pumu humpata mtoto mmoja hadi wawili katika kila watoto 10 kwa marekani. Hii ina maana kwamba kama una watoto 20 darasani, watoto 2-4 kati yao wanaweza kuwa na ugonjwa wa pumu. Ugonjwa wa pumu unaweza kumshika mtu katika umri wowote- kuanzia mtoto mchanga hadi mtu mzima-lakini huwashika zaidi watoto wenye umri wa kwenda shule(kuanzia miaka sita na kuendelea)

Hakuna anayejua kwa uhakika kwa nini ugonjwa huu unampata mtu mmoja na kuacha mwingine, lakini tunajua kwamba ugonjwa wa pumu unatokea ndani ya familia zetu. Hii ina maana kwamba kama mtoto ana pumu, yeye pia anaweza kuwa na mzazi, ndugu, mjomba au jamaa mwingine mwenye pumu au alikuwa na ugonjwa huu wakati bado mtoto.

Ugonjwa wa pumu unapoanza,huonyesha kama vile ni mafua,ambayo huambatana na kikohozi chenye kutoa mlio wa filimbi,lakini ugonjwa wa pumu siyo wa kuambukizwa. Huwezi kuambukizwa Kama unavyopata mafua

Ni sababbu zipi zinazopelekea Kupata shambulio la ugonjwa wa pumu (Asthma attack)?
Visababishi hutofautiana kutoka mtoto mmoja hadi mwingine. Sababu zipo nyingi.
❗Baadhi ya watoto huwa na mzio(allergy), kwa vile vitu ambavyo huathiri nji vya ugonjwa wa pumu

Uwezekano wa kupata ugonjwa wa pumu huongezeka iwapo mtu

Atakuwa na magonjwa ya mzio kama vile magonjwa ya ngozi (eczema) au homa isababishwayo na aina fulani ya vumbi (hay fever)
Atavuta chavu (pollen) kutoka kwenye maua au miti
Atajihusisha na uvutaji sigara
Ana historia ya ugonjwa wa pumu au mzio kwenye familia

❗Utumiaji wa dawa aina ya aspirin
Ana msongo wa mawazo
Ana uambukizi wa magonjwa ya virusi kama rhinovirus
Mazoezi
Anaishi sehemu zenye baridi
Ana matatizo katika njia yake ya chakula (Gastroesophageal reflux disease au GERD)

Dalili za ugonjwa wa pumu NI pamoja na .

❗Kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida (shortness of breath)
Kutoa sauti kama mtu anayepiga miluzi wakati wa kupumua (wheezing)

❗Kukohoa sana (chronic cough) hasa nyakati za usiku au asubuhi. Aidha kikohozi huambatana na kutoa makohozi mazito, yasiyo na rangi au yenye rangi ya njano.
Kubana kwa kifua.

Kwa mtu aliyepata shambulizi kubwa la pumu (severe asthmatic attack) anaweza kushindwa kuzungumza na pia kuwa na hali kama ya kuchanganyikiwa.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data