IFAHAMU SIRI YA MAUMIVU MAKALI WAKATI HEDHI KWA MWANAMKE

IFAHAMU SIRI YA MAUMIVU MAKALI WAKATI HEDHI KWA MWANAMKE - Tanzania
IFAHAMU SIRI YA MAUMIVU MAKALI WAKATI HEDHI KWA MWANAMKE - Tanzania
  • IFAHAMU SIRI YA MAUMIVU MAKALI WAKATI HEDHI KWA MWANAMKE - Tanzania
  • IFAHAMU SIRI YA MAUMIVU MAKALI WAKATI HEDHI KWA MWANAMKE - Tanzania
Description :

Kwanini unakuwa unapatwa na maumivu Makali wakati hedhi?
Wanawake wengi hupatwa na hali ya tumbo kuuma kama vichomi fulani kabla au wakati wanapokuwa katika mzunguko wa hedhi. Walaki pia mwanamke anaweza kupatwa na chango la tumbo.

Maumivu ya tumbo baada ya hedhi kitaalamu tunaita, “secondary dysmenorrheal”. Huwa ni hali ya kawaida kwa mwanamke anapofikia umri mkubwa. Tutaielezea baadaye kwa upana hali hii ili tujue vyanzo vyake.

Je, Unaweza Kuyahisi Vipi Maumivu?

Maumivu ya tumbo baada ya hedhi mara nyingi husikika maeneo ya tumbo la chini na mgongoni. Unaweza ukahisi maumivu pia kwenye maeneo ya nyonga na mapajani.

Hali ya maumivu haya inaweza kuambatana na kichefuchefu na maumivu ya kichwa pia. Pia unaweza ukahisi tumbo kujaa gesi, kukosa choo au kuharisha.
Maumivu yanaweza kuwa makali na yakaendelea kwa muda mrefu kuliko maumivu ya kawaida yanayojitokeza wakati wa hedhi. Maumivu yanaweza pia kuanza mapema kwenye mzunguko wako wa hedhi badala ya kuanza kabla ya kipindi cha hedhi kinachofuata.
Maumivu au vichomi hivi mara nyingi huwa sio vikali sana. Hata hivyo, ni muhimu sana kuvisikiliza hasa pale vinapokaa kwa muda mrefu.

Je, Nini Husababisha Maumivu Haya?

Wakati mwingine maumivu baada ya hedhi huwa sio makali sana. Lakini kama una maumivu yasiyo koma yanayodumu muda mrefu kuliko mzunguko wako wa hedhi, basi inaweza ikawa ishara au dalili kwamba una tatizo mwilini mwako.
Hapa nitapenda nielezee visababishi mbali mbali vya maumivu yanayompata mwanamke baada ya kutoka katika kipindi cha hedhi:

Ngozi Ya Ndani Ya Tumbo La Uzazi(Endometriosis)

Endometriosis ni ugonjwa ambao hujitokeza wakati ngozi ya juu ya tumbo la uzazi inapovimba . Hali hii inaweza kusababisha maumivu kabla, au baada ya kipindi cha hedhi. Maumivu haya yanaweza kuambatana na uvimbe au maumivu ya nyonga.

NUKUU: Maumivu yanaweza yakawa makali, na yanaweza kujitokeza wakati unapofanya tendo la ndoa au baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa au wakati unapojisaidia haja kubwa au haja ndogo. Maumivu haya endelevu unaweza kuyahisi maeneo ya tumbo la chini au mgongoni.

Dalili za ugonjwa wa Endometriosis huwa kama ifuatavyo:
Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa

Maumivu wakati unapojisaidia haja kubwa au ndogo

Kushindwa kubeba ujauzito(ugumba)

Kuhisi uchovu

Kuhara au kukosa choo

Tumbo kujaa gesi

Kichefuchefu

Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi au kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja
Maumivu ya tumbo kabla, au wakati wa hedhi au baada ya hedhi ambayo yanaweza kuambata na maumivu ya tumbo la chini au mgongoni.

Uvimbe Katika Mlango Wa Kizazi(Adenomyosis)

Adenomyosis ni uvimbe usababishwao na kuota kwa tishu zisizo za kawaida katika mlango wa uzazi. Badala ya kuota ndani ya tumbo la uzazi, tishu hizi huota kwenye mizuli ya tumbo la uzazi. Dalili zake huwa kama ifuatavyo:

Kutokwa na damu muda mrefu wakati wa hedhi

Kuhisi maumivu makali ya nyonga wakati wa hedhi

Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa

Damu kuganda wakati wa hedhi

Kuhisi kitu kigumu maeneo ya tumbo la chini.

Maambukizi Katika Via Vya Uzazi Au PID.

Ugonjwa wa PID kama tulivyokuwa tujifunza siku zote, husababishwa na bakteria ambao huambukiza viungo vya uzazi. Bakteria hawa wanaweza kuenea kutoka kwenye uke na kuelekea kwenye tumbo la uzazi, vifuko vya mayai, au mirija ya uzazi.

Hayo ndio maeneo ambayo huathiriwa sana na maambukizi katika via vya uzazi ikiwa kama tatizo hilo halitatibiwa mapema.

PID inaweza isionyeshe dalili hapo mwanzo. Lakini baadaye dalili zinaweza kuonekana nazo huwa kama ifuatavyo:

Maumivu ya nyonga au ya tumbo la chini
Kutokwa na uchafu mwingi ukeni
Kutokwa na damu nyingi wakati wa unapofanya tendo la ndoa
Kuhisi kama vile una homa au mafua
Kushindwa kukojoa kwasababu ya maumivu
Tumbo kuunguruma. Hivyo kwa ujumla maumivu haya wakati wa hedhi huwa NI kawaida kwa mwanamke lakini pale yanapo kuwa too much wakati mwingine kunakuwaga na chanzo chake .
Kwahyo siyo Kila maumivu wakat wa hedhi NI ya kawaida.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data