FANGASI SEHEMU ZA SIRI

FANGASI SEHEMU ZA SIRI - Tanzania
FANGASI SEHEMU ZA SIRI - Tanzania
 • FANGASI SEHEMU ZA SIRI - Tanzania
 • FANGASI SEHEMU ZA SIRI - Tanzania
Description :

*FANGASI UKENI DALILI ZAKE VISABABISHI NA MATIBABU*Mamilioni ya watu kwa sasa wanapambana na kiumbe mwenye seli moja asiyeonekana, ambaye ni fangasi anayeitwa Candida.  Maambukizi ya fangasi ukeni imekuwa ni tatizo kubwa sana duniani
Asilimia 75 ya wanawake wote duniani wanasumbuliwa na tatizo hili na wanatafuta dawa ya fangasi ukeni kila siku. Maambukizi haya ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke yakisababishwa kwa kiasi kikubwa  na fangasi aina ya Candida Albicans, na maambukizi haya pia hujulikana kama Yeast infection/Yeast thrush.

Fangasi Ukeni Husababishwa Na Nini? Je Kuna tiba?

Kikawaida vimelea hawa wa Candida Albicans hupatikana katika midomo, mpira wa kupitishia chakula (Pharynx), kibofu cha mkojo, uume au katika uke na kwenye ngozi pia.
Bacteria hawa huishi katika sehemu hizo bila kuleta  madhara isipokua pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika. Mfano mabadiliko katika hali ya PH, tutambue PH ya mwanamke ndani ya uke ni 4.0-4.5 au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine, hivyo huharibiwa kutokana na sababu mbalimbali.

Kupungua kinga husababisha fangasi ukeni

Pia kupungua kwa Kinga ya mwili kutokana na magonjwa mbalmbali huletekeza kukua kwa Candida, ndio maana wagonjwa wenye maradhi ya ukimwi na saratani ama wanaopata matibabu ya mionzi huwa kwenye hatari kubwa ya kuumwa fangasi ya Candida.
Candida pia hupatikana kwenye mdomo, tumbo, kwenye kwapa,  hivo pale inapotokea fangasi hawa wa Candida kuanza kukua kupita kiasi bila kudhibitiwa kitendo hicho huitwa Candidiasis ama Yeast infection,matokeo yake ni mfululizo wa maambukizi na kuumwa kwa mwili .

Taarifa sahihi kuhusu ugonjwa

Bahati mbaya ni kwamba taarifa nyingi za mtandaoni zimekuwa zikipotosha pasipo kueleza kwa ufasaha juu ya tatizo hili na hivo kufanya uelewaji wa tatizo kuwa mgumu. Hivo kama unasumbuliwa na tatizo hili na unapenda kujifunza na unahitaji kujua kuhusu dawa asili ya fangasi sugu basi endelea kusoma makala hii kwa umakini mpaka mwisho.
Ni muhimu kuelewa kwamba kukua kupita kiasi kwa Candida siyo kwasababu Candida wanapatikana kwenye eneo husika, hapana na ndio maana tatizo linakuwa gumu kutibika kutokanana na kwamba dawa nyingi huua Candida wote na kuua bacteria wazuri na hivo kuharibu msawazo wa mwili. Kumbuka uwepo wa Candida ni muhimu kwa ufanisi wa mwili.

Fangasi Ukeni (Vaginal Candidiasis)

Maambukizi ya fangasi ukeni yanaweza isiwe ugonjwa hatari pale unapoanza, lakini huleta usumbufu na harufu kali na hivo mgonjwa kukosa amani. Baadhi ya mambo yanayoongeza hatari ya kupata maambukizi ya fangasi ukeni ni ujauzito, kuumwa kisukari, kushuka kwa kinga ya mwili kutokana na kuugua magonjwa mbalimbali na pia matumizi yaliyokithiri ya dawa hasa zile za kuua bacteria/antibiotics.
Wanawake wapo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua fangasi za sehemu za siri ukilinganisha na wanaume, lakini pia hata wanaume huambukizwa tatizo hili.

Je Upo Kwenye Makundi ya Tabia hizi Hatarishi Kupata Fangasi Ukeni?

Kwa wanawake kuna baadhi ya tabia hatarishi zinazoongeza chansi ya kupata maambukizi ya fangasi wa Candidiasis.

ngono mara kwa mara na watu tofauti tofauti bila kinga

kufanya ngono kupitia mdomo

matumizi makubwa ya kondomu wakati wa ngono

matumizi makubwa ya tissue za kujisitiri/ huitwa pantliners

Mambo mengine hatarishi yanayopelekea fangasi

matumizi yaliyokithiri ya antibiotics

kuugua kwa mda mrefu ugonjwa wa Kisukari.

kiwango kikubwa cha homoni za uzazi.

vinasaba na

uvutaji wa sigara

Hatua za maambukizi ya fangasi ukeni

1.Maambukizi yasiyo makali(uncomplicated thrush)
Katika aina hii mgonjwa hupatwa na maambukizi mara moja hadi nne kwa mwaka pia dalili zake huwa si za kuogopesha na maambukizi haya husababishwa na fangasi aina ya Candida Albicans.
2.Maambukizi makali (complicated thrush)
Katika kundi hili mgonjwa hupatwa na maambukizi mara nne au zaidi kwa mwaka. Pia dalili zake huwa ni za kuogopesha kama maambukizi yatakua yametokea kipindi cha ujauzito, ugonjwa wa VVU

Our safety tips

 • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
 • At all costs, avoid paying before seeing the item.
 • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
 • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
 • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
 • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
 • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data