FAHAMU UGONJWA WA UTI, DALILI NA JINSI YA KUEPUKA UTI SUGU
UTI(Urinary tract infection) ni ugonjwa wa maabukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya yanasababishwa na viumbe kama bakteria,fangasi na virus. Maranyingi bakteria wanaoingia kwenye mfumo wa mkojo hutolewa na mwili,Wakati mwingine bakteria wanaweza zidi kinga ya mwili na kusababisha maambukizi hayo.
UTIs inaweza athiri urethra,kibofu cha mkojo na figo
MFUMO WA MKOJO
Mfumo wa mkojo ni mfumo wa mwili unaotumika kuondoa uchafu na maJi ya ziada
Mfumo huu unaundwa na ureta,kibofu cha mokojo,figo na urethra sitachambaua kwa undani hizi sehemu
KISABABISHI CHA UTI
Mara nyingi UTI zinasababishwa na bakteria aitwaye Escherichia coli (E. coli) na UTI nyingine zinaweza sababishwa na Chlamydia na Mycoplasma na UTI hizi zina athiri hadi mfumo wa uzazi na wanandoa wanapaswa kupata tiba pamoja,
Maambukizi ya UTI ni makubwa sana dunian Zaidi ya watu milioni 8 pointi 1 wanaathiriwa na ugonjwa huu
KWANINI WANAWAKE NDO WAHANGA WAKUBWA?
Wanawake ni wahanga wakubwa sana wa ugonjwa huu kulingana na maumbile yao ya nje
1.Urethra(mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu) kwa wanawake ni mfupi sana hivyo kuruhusu bakteria kufika kwa haraka kwenye kibofu
2.Pia mrija huo unafungukia sehemu ambazo zinaweza kuwa ni vyanzo bakteria ambayo ni sehemu ya uke na pili ni puru
Kwa wanaume ni vigumu sana ila wakipata tatizo linaweza kuwa zito kutibu tofauti na kwa wanawake
WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA UTI
#Watu wenye vidonda kwenye uti wa mgongo
#Mtu yeyote mwenye tatizo katika mfumo wa mkojo
#Tendo la ndoa linaweza likahamisha bakteria kutoka kwenye uke kwenda kwenye urethra
#Baadhi ya njia za uzazi kama kutumia diaphragm,spermicides,kondomu nk
KURUDIARUDIA KWA UTI(UTI SUGU)
Mara nyingi wanawake wakipata UTI inaweza ikawa inajirudia mara kwa mara kulingana na sababu zifuatazo
1.Uwezo wa bakteria kujishika kwenye njia ya mkojo hivyo kutotibika na kurudia tena
2.Sababu nyingine ni wanawake kuwa non sector yani kuwa na damu grupu A,B na AB ambao hawawez kuzalisha kinga nzur kwa ajili ya hao bakteria
DALILI ZA UTI
1.Kukojoa mara kwa mara na maumivu wakati wa kukojoa
2.Kuhisi kuunguzwa na mkojo kwenye kibofu au mrija wa mkojo
3.Maumivu ya misuli na tumbo
4.Mkojo kuwa na harufu mbaya na pia kubadilika rangi kuwa nyeusi au rangi ya mawingu nk
5.Kwa mtu aliyeathiriwa figo anaweza kuwa na maumivu mgongoni au kwenye mbavu pia kichefuchefu na kutapika
6.Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo unatoka kidogo
JINSI YA KUZUIA UTI SUGU
1.Kunywa maji mengi kunsaidia kusafisha bakteria kwenye mfumo
2.Mtu anatakiwa akojoe mara kwa mara kila anapojiskia kukojoa
Mkojo ukikaa sana kwenye kibofu unaweza zalisha bakteria
Na baada ya kukojoa wanawake wanatakiwa kujisafisha kuanzia mbele kurudi nyuma ili kulinda urethra
3.Vaa nguo za ndani za pamba na ambazo hazibani sana kuruhusu hewa kupita vizuri ,epuka jinsi zinazobana sana ambazo zinaweza kukusanya na kuleta tatizo.
Karibu kwa ushauri zaidi kama imekuwa sugu na kujirudia.
FAHAMU UGONJWA WA U.T.I KIUNDANI
Description :
Our safety tips
- Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
- At all costs, avoid paying before seeing the item.
- Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
- Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
- If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
- Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
- Beware of offers that are too good to be true.
This listing was not posted by a representative of Jumia. Jumia cannot guarantee the origin of the product / service.