FAHAMU MBINU JINSI YA KUMSAIDIA MTOTO ANAYEKATAA KULA NA SABABU ZAKE.U

FAHAMU MBINU JINSI YA KUMSAIDIA MTOTO ANAYEKATAA KULA NA SABABU ZAKE.U - Tanzania
  • FAHAMU MBINU JINSI YA KUMSAIDIA MTOTO ANAYEKATAA KULA NA SABABU ZAKE.U - Tanzania
Description :

Kwanini watoto wanakataa chakula ?
Ili kuweza kutatua tatizo ni vizuri kutafuta kitu kinachosababisha tatizo, je kwanini watoto wengine wanakataa kula ?

Mie sikuwa na jibu la haraka, bali nikaona ni vizuri kwenda kumuona daktari bingwa wa masuala ya watoto ambaye ameshakutana na matatizo mengi kama haya. Daktari alisema kuwa kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kumfanya mtoto akatae kula, hizi hapa ni chache tu:

Mtoto anakuwa ameshiba na hajisikii hamu ya kula. Hii inawezekana kusababishwa na mtoto kula vitu vidogo vidogo mara nyingi hivyo kuzuia njaa na kumzuia kula chakula vizuri.
Hapendi chakula anachopewa sababu hajakizoea au hakifurahii. Watoto wengi wanaweza kukataa kula mboga za majani, lakini ni muhimu sana ale sababu ni chakula pekee kinachomfanya akue vizuri.
Anaumwa na amepoeza hamu ya kula. Ugonjwa ni moja ya sababu kubwa za kumfanya mtoto kugoma kula.
Amechoka chakula anachopewa hivyo kutokifurahia tena. Kula chakula cha aina moja muda mrefu inaweza kuwa ni sababu kubwa ya mtoto kugoma kula. Hata kama anafurahia chakula, wakati mwengine anaweza asipende tena kula. Hivyo ni vizuri kuweka vyakula tofauti ili mtoto apate ladha na virutubisho tofauti.
Ni muhimu kuzingatia kuwa, katika mazingira yeyote yale usimlazimishe mtoto kula na ni hatari kubwa kumkaba ili ameze chakula. Kulazimisha mtoto kula ni kumjengea tabia ya kuchukia chakula. Mtoto akishajenga tabia hii hawezi kuacha sababu atakuwa anahusisha chakula na adhabu. Sababu hakuna mtu anayependa adhabu, atakuwa anachukia chakula cha aina yeyote. Matokeo yake ni kuwa mtoto atajenga tambia mbaya zaidi ya kukataa kula chakula cha aina zote. Pia, kumkaba mtoto kunaweza kuleta matatizo makubwa kama vile kufanya chakula kuingia kwenye njia ya hewa, hii itakuletea kesi zisizo za lazima.

Jinsi ya kutatua tatizo
Kutatua tatizo huanzia kwenye kujua tatizo liko wapi. Ushauri nasaha aliotoa daktari ni kuwa, hakuna muarobaini wa kutibu hii tabia, bali ni swala la kujaribu mbinu mbalimbali ili kuweza kujua kitu kimoja kinachoweza kuwa suluhisho la ukataaji wa kula wa mtoto.

Katika njia muhimu alizopendekeza ni pamoja na hizi hapa:

1. Kubadilisha vyombo vya chakula vya mtoto


Daktari alisisitiza kuwa, mtoto huvutiwa zaidi na rangi, hasa kwenye vitu anavyotaka kula. Mtoto anaweza kuchoka kula chakula sababu anatumia chombo kimoja kila siku, hii haijalishi kama chakula kinabadilika au la. Ni muhimu kumuandalia mtoto chakula kwenye vyombo vyenye rangi na maumbo tofauti. Na ushauri wa daktari ni kuwa, usirudie chombo kwa wiki nzima, kama inawezekana. Hii inamfanya mtoto kuona utofauti wakati wa kula, na kumfanya apate hamu ya kula.

Mfano, unaweza kutumia bakuli, vikombe, sahani, vijiko vyenye rangi tofauti ili kumfanya aone anakula katika mazingira tofauti na hii humfanya awe na hamu kula chakula zaidi.

2. Watoto wale pamoja na familia


Watoto hupenda kuiga wazazi. Mara nyingi sana watoto hupewa vyakula wale wakiwa wenyewe wakati watu wengine wanaendelea na shughuli za kawaida. Hii inaweza kumfanya mtoto kupendelea zaidi kucheza kuliko kula. Ni muhimu kumlisha mtoto wakati familia nzima imekaa mezani au jamvini tayari kwa kula. Katika muda huu mtoto atakula vizuri bila vikwazo, maana kila mmoja anakula.

Vilevile, watoto wengine (umri wa miezi 10 hadi miaka 2) hupendelea kula vyakula wanavyokula watu wazima, hata kama haviwafai, na kugoma vyakula vya watoto. Ni bora kumuandalia chakula kinachofanana na unachokula wewe na kumpa ili apate kufurahia. Huwezi kubishana na mtoto, ingawa huwezi kumpa kila kitu anachotaka pia. Ila jaribu kutumia mbinu tofauti ili apate kula na kuridhika. Afya yake ni bora kuliko kitu kingine kwenye maisha yake kwa muda huu.

3. Jaribu kumsoma mtoto anapenda nini


Kila mzazi ana jukumu la kumsoma mwanae anapendelea nini. Ili kuweza kumfanya mtoto ale vizuri, ni vyema kubadilisha vyakula kila wakati – siyo kila siku. Mara nyingi watoto huchukua muda kuzoea chakula, hivyo ni vizuri kumpa mtoto chakula kwa muda wa siku 2 hadi 3 na kumbadilishia .

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data