Fahamu Kuhusu Tezi Dume/ Prostate

Fahamu Kuhusu Tezi Dume/ Prostate - Tanzania
Fahamu Kuhusu Tezi Dume/ Prostate - Tanzania
  • Fahamu Kuhusu Tezi Dume/ Prostate - Tanzania
  • Fahamu Kuhusu Tezi Dume/ Prostate - Tanzania
Description :

TEZI DUME NI ✍️?✍️?✍️?.
tezi dume ni kiungo tu kama vilivyo viungo vingine kwenye mwili, mfano moyo, ini, figo na viungo vingine. Ila tezi dume ni kiungo kinachopatikana kwa mwana damu mwanamume tu, ndio maana ikaitwa tezi dume.

Kwa kawaida binadamu tuna tezi mbalimbali kwenye mwili, mfano pituitari , thairoidi, kongosho, na tezi zingine.

Kuna baadhi ya tezi huwa zinapatika kwa wote yaani mwanamke na mwanamme. Mfano kongosho, pituitari, thairoidi.

Lakini kuna baadhi ya tezi zinapatikana kwa jinsia moja tu, mfano ovari inapatikana kwa wanawake tu na tezi dume (prostate gland) inapatikana kwa wanaume tu.

Hivyo binadamu yoyote wa kiume anayo tezi dume (prostate gland) moja kwenye mwili wake.

UMUHIMU WA TEZI DUME.
1. Tezi dume huzalisha maji maji ya maziwa yanayopatikana kwenye shahawa. Maji maji hayo husaidia kulinda mbegu za mwanaume zisiharibike au kufa wakati wa kutoka nje na kuingia kwenye uke.

2. Wakati wa kumwaga shahawa (ejaculation), tezi dume husinyaa (contracts) na kuminya mlija wa mkojo, ndio maana haiwezekani kukojoa na kumwaga shahawa (ejaculation) kwa pamoja.

kama viungo vingine vinavyoweza kupata shida, basi hata tezi dume inaweza kupata shida. Mfano unaweza kupata shida ya jino kuuma au kulegea, basi pia tezi dume huwa inapata shida hasa wakati wa uzee. Shida hizo ni:

1. TEZI DUME KUONGEZEKA UKUBWA (BENIGN PROSTATE HYPERTROPHY).
Tezi dume inaweza kuongezeka ukubwa na kusababisha shida nyingine kwenye mwili ikiwemo matatizo ya kushindwa kukojoa (yaani mkojo kushindwa kutoka nje).

2.SARATANI YA TEZI DUME. (PROSTATE CANCER)
Mwanaume anaweza kupata saratani ya tezi dume, yaani seli za tezi dume zikajizalisha kwa wingi na bila mpangilio maalumu, hivyo tezi dume ikakua kwa kiwango kikubwa. Hii inaweza kupelekea shida mbali mbali, ikiwemo shida ya mkojo lakini pia saratani ikasambaa katika viungo vingine vya karibu mfano , kibofu cha mkojo na utumbo mpana...

USHAURI NA TIBA.
Endapo utapata Dalili hizi unashauliwa kuonana na Daktari kwa ajiri ya vipimo , dalili Kama kukojoa Mara kwa Mara ,mkojo usioisha , maumivu wakati wa kukojoa , kukojoa Mara kwa Mara nyakati za Usiku , Kujikojoloea, maumivu ya viungo, kushindwa kusimamisha uume vizuri wakati wa tendo la ndoa "Erectile desfunction", pamoja na Damu katika mkojo "blood urine", pia tunazo dawa za asili naturalceutical ambazo zinatibu changamoto hizi za tezi dume bila operation.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data