FAHAMU CHANZO NA SABABU ZA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA MWANAMKE NA MWANAUME

FAHAMU CHANZO NA SABABU ZA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA MWANAMKE NA MWANAUME - Tanzania
  • FAHAMU CHANZO NA SABABU ZA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA MWANAMKE NA MWANAUME - Tanzania
Description :

KUWASHWA sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani kujumuisha maradhi ya uke kwa wanawake au muwasho na kuvimba kwa sehemu za siri za wanaume (jock itch). Bila kujali jinsia muwasho unaweza kusababishwa na ugonjwa wa ngozi, magonjwa ya zinaa au mzio (allery).

Watu wengi wamekuwa na tatizo la muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu f’lani na huisha wenyewe baada ya kitu hicho kuondolewa, vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi, ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari.

Nini husababisha muwasho sehemu za siri za mwanaume?
Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu zingine za mwili. Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndiyo chanzo kikuu cha kuwashwa uume. Sababu zingine ni maradhi ya fangasi, ugonjwa wa upele (scabies), kuwepo kwa chawa, mzio, maambukizi ya bakteria n.k
Nini husababisha muwasho wa sehemu za siri kwa mwanamke?

(i) Maambukizi ya Fangasi Ukeni (Vaginal Yeast Infection) ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosababishwa na fangasi waitwao Candida. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.
Usikose kufuatilia makala haya wiki ijayo.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data