EPUKA VYAKULA HIVI KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO

EPUKA VYAKULA HIVI KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO - Tanzania
  • EPUKA VYAKULA HIVI KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO - Tanzania
Description :

VYAKULA AMBAVYO MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO HATAKIWI KULA

Mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni lazima uwe makini sana na chakula unachokula kila siku.

Chakula unachokula kila siku kitaamua ikiwa dawa unayotumia kutibu vidonda vya tumbo itakuponya na kukuacha huna vidonda tena milele au ndiyo utapata nafuu ya muda mfupi tu na baadaye utaendelea kuumwa vidonda tena na tena mpaka utakapo kata tamaa na kutoamini kama hakuna kupona vidonda vya tumbo.

Chakula unachokula kinapaswa kiwe ni dawa.
Usile tu ili kushiba au kwa sababu unasikia njaa. Lazima ujuwe hiki unachokula ni nini, kina kazi gani mwilini na je kinaweza kusaidia kupona au kupunguza makali ya vidonda vya tumbo?

Hiki unachokula ni nini?

Kina kazi gani mwilini?

Je kinaweza kusaidia japo kupunguza gesi au kupunguza asidi tumboni na kutibu vidonda au majeraha tumboni?.

Kanuni ya jumla ya chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo kwa siku ni kuwa asilimia 80 ya chakula unachokula katika siku iwe ni mboga za majani na matunda.

Hii ni kusema kama jumla ya chakula unachokula kwa siku kina ujazo wa kilo 3 basi kilo 2 na nusu ziwe ni matunda na mboga za majani na nusu kilo iliyobaki ndiyo viwe vyakula vingine.

Cha kwanza kabisa unapoamka kitandani asubuhi, yaani ile unatua tu mguu kutoka kitandani ni maji ya kunywa.

Ukiamka tu kabla hata ya mswaki unapaswa unywe maji glasi moja (robo lita) au glasi 2 (nusu lita) ndiyo uendelee na maandalizi ya chai na kupiga mswaki na shughuli zingine.

Na hii ni kwa wote haijalishi unaishi sehemu zenye baridi au joto ni lazima kunywa maji.

Maji ya kawaida siyo ya kwenye friji wala siyo ya moto au ya uvuguvugu.

Maji ya kawaida (room temperature).

Soma hii pia > Vyakula vya asubuhi vya mgonjwa wa vidonda vya tumbo

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula

1. Vyakula vya kusisimua
Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo.
Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua kama vile ketchup, chill sauce, tomato sauce, achali, pilipili na vingine vingi vya jamii hii huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni.

Sababu ni kuwa, visisimuaji hivi huzichoma pia kuta za tumbo na kuongeza zaidi vidonda vya tumbo.

2. Vinywaji na vyakula vyenye kaffeina na asidi nyingi.
Vinywaji vyenye kaffeina na asidi nyingi kama vile chai ya rangi, kahawa, soya sauce, mayonnaise, jibini, Vyakula jamii ya Mkate, samaki wa kwenye makopo, pombe, soda na juisi za viwandani pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kutokea kwa vidonda vya tumbo.

3. MAZIWA Fresh
Kwa miaka mingi watu wenye vidonda vya tumbo wamekuwa wakihimizwa kunywa maziwa kwa wingi kwa matumaini kwamba yanaponyesha vidonda vya tumbo.

Utafiti wa karibuni umebaini maziwa si salama kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo.

Kwahiyo kama umekuwa ukinywa vikombe na vikombe vya maziwa kwa matumaini unajiponya vidonda vya tumbo habari hii haikuachi salama

Ndiyo ukinywa maziwa unaweza kusikia nafuu fulani kwa dakika kadhaa lakini baadaye hubadilika na kuwa mbaya zaidi.

Ni vizuri zaidi kunywa maziwa mtindi kuliko maziwa freshi. Mtindi una bakteria wazuri mhimu kwa ajili ya tumbo na kinga ya mwili

Unajuwa imefika mahali watu hawaamini kama kuna dawa ya kuponya vidonda vya tumbo.Wengine hawaamini kabisa kama huu ugonjwa unatibika.

Lakini uchunguzi wangu umebaini wengi wanatumia dawa lakini hawajuwi wale nini na nini wasile.

Vidonda vya tumbo ili upone siyo dawa hasa, mhimu ni kujua nini ule na nini usile kwa kipindi kirefu kisichopungua miezi 6.

Kwa sehemu kubwa vidonda vya tumbo ni matokeo ya asidi kuzidi tumboni kwa muda mrefu mfululizo bila wewe kujua. Kwa sababu hii kuendelea kunywa tena na tena maziwa katika siku kunapelekea kuundwa kwa hydrochloric acid ambayo ni chanzo pia cha vidonda vya tumbo

PATA TIBA YA ASILI YA VIDONDA WASILIANA NASI na KUPATA MWONGOZO WA KUJITIBU

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data