DAWA YA UGONJWA WA MAWE KWENYE FIGO BILA UPASUAJI

DAWA YA UGONJWA WA MAWE KWENYE FIGO BILA UPASUAJI - Tanzania
  • DAWA YA UGONJWA WA MAWE KWENYE FIGO BILA UPASUAJI - Tanzania
Description :


Ugonjwa Sugu wa Figo: Dalili na Utambuzi
Dalili na utambuzi wake.

Katika hali hii ya ugonjwa sugu wa figo, figo hushindwa kufanya kazi polepole,kwa miezi hata miaka kwa hiyo mwili huzoea hatari za hali hii. Pia, figo huwa na uwezo mkubwa wa kujisaidia katika shida ya kazi zake.kwa sababu hizi mbili, watu walio na ugonjwa huu usiopona huwa hawana dalili zozote hadi wakati figo zimeharibika sana.

Figo huwa na kazi nyingi sana kama kutoa uchafu na maji kwenye mwili, kuzuia shinikizo la damu,kusawazisha kemikali mwilini , uzalishaji wa chembechembe za damu nyekundu mwilini na kadhalika.Hivyo kutegemea matatizo yaliyoko kwenyefigo, dalili huwa tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine katika ugonjwa sugu wa figo.

Dalili za ugonjwa sugu wa figo ni zipi?

Dalili hutofautiana kulingana na kiwango cha ugonjwa.Ili kuelewa vyema na kukabiliana na hali hii vizuri,ugonjwa wa figo umegawanywa katika viwango vitano kulingana na kiasi cha utoaji uchafu kwenye figo (Glomerular Filtration Rate- GFR),ambacho ndio kiwango cha kuonyesha jinsi figo zinavyochuja uchafu kutoka kwenye damu.GFR huhesabiwa kulingana na kiasi cha creatinini kwenye kipimo cha damu. Kipimo cha GFR ni kipimo sahihi cha kuonyesha utendaji wa figo: Utendaji mzuri wa figo ni wakati GFR ni zaidi ya mililita tisini kwa kila dakika (90 ml/min).

Mapema katika ugonjwa huu,(CKD) wagonjwa wengi hawana dalili zozote za ugonjwa.
Hatua za ugonjwa wa figo usiopona.
HatuatHatua Ya kwanzatHatua Ya pilitHatua Ya tatutHatua Ya nnetHatua Ya tano
tGFR ya KawaidatKiwango kidogo cha ugonjwa wa figotUgonjwa kiasi cha figotUgonjwa mkali wa figotHatau za za mwisho
GFRtZaidiya 90 ml/dakikat60-89 ml/dakikat30-59 ml/dakikat15-29 ml/dakikatkidogo kuliko 15 ml/ dakika


Hatua ya kwanza ya ugonjwa wa figo usiopona (kazi ya figo ikiwa 90_-100%)

Hii ni hatua ya mapema ya ugonjwa huu na figo huwa hazijadhurika. Umajimaji (serum creatinini) kwenye damu huwa uko katika kiwango cha kawaida.Katika hatua hii ya kwanza ya CKD tatizo linaweza tu kujulikana mtu anapofanyiwa uchunguzi wa kimatibabu au anapopimwa kwa ugonjwa mwingine.

Ishara za hali hii zinaweza kukosekana. Kwa mfano;kuwepo kwa protini kwenye mkojo, sura yafigo kuonekana zimebadilika kwenye picha za eksirei, ultrasound,MRI au CT,historia ya familia yenye ugonjwa wa uvimbe wa figo (polycystic kidney).

Hatua ya pili ya ugonjwa wa figo usiopona (kazi ya figo ikiwa 60_89%)

Hapa figo zimedhurika kidogo.Wagonjwa wanaweza kuwa hawana dalili, lakini ishara zinaweza kuwa ni kukojoa mara nyingi hasa usiku,shinikizo la damu kuwa juu,mkojo usio wa kawaida na creatinini kwenye damu inaweza kuwa juu ( au hata kawaida).

Shinikizo la damu katika umri mdogo ni ishara kuu ya ugonjwa wa figo.
Hatua ya tatu (kazi ya figo ikiwa 30_59%)

Ugonjwa huwa na kasi,wagonjwa wanaweza kuwa hawana dalili au wana dalili kidogo pamoja na mkojo kuwa si wa kawaida,na creatinini kwenye damu kuongezeka.

Hatua ya nne (Kazi ya figo ikiwa 15_29%)

Katika hatua hii ya ugonjwa, ugonjwa huwa mkali. Kuna dalili nyingi, kutegemea chanzo cha kudhoofika kwa figo na magonjwa mengine yaliyoambatana na hali hii.

Hatua ya tano(kazi ya figo ikiwa kidogo chini ya 15%)

Hii ni hatua ya mwisho na ni ya hatari.Kuna dalili nyingi na nyingine zinazohatarisha hata maisha.Katika hatua hii hata matibabu yakifanywa,dalili za figo kufeli huzidi na wagonjwa wengi huhitaji dayalisisi au kupatiwa figo nyingine.

Ishara kuu za ugonjwa wa figo ni:

Kukosa hamu ya chakula,kichefuchefu na kutapika.
Kuwa mdhaifu,mwili kuchoka na kupungua uzito.
Kuvimba miguu,mikono au/na usoni karibu na macho.
Shinikizo la damu lisilozuilika hasa kwa umri mdogo.
Kukosa nguvu kunakosababishwa na upungufu wa damu mwilini (anaemia),hali inayosababishwa na figo kutotengeneza homoni ya erithropoyetini inayosaidia kutengeneza chembechembe za damu.
Kushindwa kulala,kizunguzungu na kushindwa kuwa makini.
Kukosa nguvu,kukosa hamu ya chakula,kichefuchefu na kuvimba

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data