Dawa ya PID

Dawa ya PID - Tanzania
  • Dawa ya PID - Tanzania
Description :

Pelvic inflammatory disease (PID) ni maambukizi ya viungo vya uzai vya mwanamke. Mara nyingi husababishwa na magonjwa ya ngono. Dalili zake ni ikiwemo ya maumivu chini ya tumbo na uke kutema majimaji yenye halufu mbaya. Matibabu ya haraka ya PID, mara nyingi huwa ni antibiotics, husaidia kuzuia matatizo kama ya ugumba. Mwenzi wako anatakiwa kupimwa na kutibiwa pia.

Pelvic inflammatory disease (PID) ni nini?
Pelvic inflammatory disease, au PID, hutokea kipindi viungo vya uzazi vya mwanamke vimepata maambukizi, Mfumo wa uzazi wa mwanmke ni sehemu ya mwili wa mwanamke inayohusika kwenye kubeba mimba na kupata mtoto.

Viungo vya uzazi vinavyoathiriwa na PID ni uterus, ovari na mirija ya falopian. Kipindi una PID, utahisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu. Pia unaweza kutokwa na majimaji yasiyo ya kawaida kutoka kwenye uke wako.

Unapataje PID?
Watu wengi hupata PID kupitia ngono isiyo salama, hata hivyo 15% ya maambukizi haya hayaenezwi kwa njia ya ngono. Ngono inaweza kuruhusu bakteria kuingia kwenye mfumo wa uzazi, ambapo wanaweza kuathiri viungo.

Je, naathirika vipi na ugonjwa wa PID (pelvic inflammatory disease) ?
PID inaeweza kuharibu maeneo ya mfumo wako wa uzazi, yakiwemo uterus, ovari, na mirija ya falopian. PID inaweza kuwa mbaya na kufanya upate shida ya kubeba mimba siku za usoni. PID pia inaweza kuleta kifurushi cha maambukizi kwenye nyonga kinachoitwa tubovarian abscess (TOA) ambayo, kama hakijatibiwa inaweza kufanya watu waumwe sana.

Nini kinacho sababisha pelvic inflammatory disease (PID)?
Bakteria wanaoingia kwenye njia ya uzazi mara nyingi husababisha PID (pelvic inflammatory disease). Bakteria hawa hupita kutokea kwenye uke(vagina), kupitia kwenye cervix, hadi kwenye uterus, mirija ya falopian na ovari, na kwenye nyonga.

Kawaida, bakteria wanapoingia kwenye uke, cervix huzuia wasisambae ndani zaidi kwenye viungo vingine vya uzazi. Lakini muda mwingine, cervix hupata maambukizi kutokana magonjwa yaenezwayo kwa kwa ngono STI kama gonorrhea na chlamydia. Ikitokea hali hiyo, cervix haiwezi kuzuia bakteria wasiingingie ndani zaidi.

Ugonjwa wa gonorrhea na chlamydia ambao haukutibiwa husababisha takribani 90% za kesi za PID. Sababu nyingine ni ikiwemo:

Kutoa mimba.
🌿Kujifungua mtoto.
🌿Upasuaji kwenye shingo ya kizazi.
🌿Uingizwaji wa kifaa cha mkojo, 🌿insertion intrauterine device (IUD), Hatari ni kubwa kwenye wiki chache za mwanzo baada ya insertion. Nyakati nyingi maambukizi haya huzuiliwa kwa kufanya vipimo vy magaonjwa ya zinaa kipindi cha uwekwaji wa IUD.

Dalili za PID ni zipi?
Unaweza usigundue kama una PID. Dalili zinaweza zikawa za kawaida au usizigundue. Lakini pia dalili za PID zinaweza kuanza ghafla na haraka. Zinaweza kuwa:

🍏Maumivu kwenye tumbo au chini ya kitovu, dalili kubwa na maarufu.
🍎Kutokwa na maji maji yasiyo ya kawaida ukeni, mara nyingi huwa na rangi ya manjano au kijani yakiambatana na harufu isiyopendeza.
🍏Homa
🍎Kichefuchefu na Kutapika
🍏Maumivu kipindi cha kujamiiana.
🍎Maumivu wakati wa kukojoa
🍏Mpangilio wa hedhi kuvurugik, au kutokwa na damu kidogo sana au kupatwa maumivu ya hedhi mwezi mzima.
🍎Maumivu upande wa juu kulia wa tumbo (right upper abdomen), si mara nyingi.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data