Dawa ya kupunguza uzito,mwili na nyama uzembe

Dawa ya kupunguza uzito,mwili na nyama uzembe - Tanzania
Dawa ya kupunguza uzito,mwili na nyama uzembe - Tanzania
  • Dawa ya kupunguza uzito,mwili na nyama uzembe - Tanzania
  • Dawa ya kupunguza uzito,mwili na nyama uzembe - Tanzania
Description :

KUPUNGUZA TUMBO, KITAMBI
Katika jamii yetu wanawake ndio wanaohangaika zaid kutoa matumbo yao makubwa, utawasikia mara nyingi wakiulizia kuhusu dawa ya kupunguza tumbo kwa wanawake, lakini si kwa ajili ya kukwepa madhara ya kiafya, bali kwa ajili ya kuboresha mwonekano wao kiurembo-kwao ni suala la urembo tu na si suala la afya. Kwa upande mwingine akina baba huona fahari kuwa na vitambi, kwao kitambi ni dalili ya kunyookewa na maisha.
Katika mada ya leo tutazungumzia hayo matumbo makubwa na vitambi ambapo tutaona matumbo hayo au vitambi hivyo ni nini, tutaeleza madhara ya kuwa na matumbo hayo makubwa na mwisho kutoa ushauri wa jinsi ya kuyapunguza matumbo hayo.
Nini Maana Ya Tumbo Kubwa Au Kitambi
Leo utasikia neno la ajabu kuwa “kila mtu ana kitambi, hata yule ambaye tumbo lake kwa nje linaonekana kuwa flat kabisa na kuwa kitambi kina madhara makubwa kwa afya yako kuliko aina nyingine yo yote ya mafuta yaliyo ndani ya mwili wako.”
Hii ina maana gani?
Kitambi ni mafuta na mafuta haya yanaweza kuwa chini ya ngozi yako au ndani kabisa kuzunguka moyo, mapafu, maini na viungo vingine. Ni mafuta haya ya ndani (visceral fat) ambayo yanaweza kuwa tatizo kubwa kwa afya yako hata kama mwili wako ni mwembamba kiasi gani. Mwili huhitaji mafuta haya ya ndani kwa ajili ya kutenganisha viungo vya ndani ya mwili visigusane na kusuguana, lakini yakizidi huleta matatizo ya kiafya. Ukiwa na mafuta mengi mno utakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa kama ya high blood pressure, kisukari (Type 2 Diabetes), magonjwa ya moyo, kansa (kansa ya maziwa na kansa ya utumbo) na mengine. Kuongeza uzito au kunenepa kunasababisha mwili ushindwe kupata sehemu ya kutosha ya kuhifadhi mafuta na hivyo kuanza kuyatunza mafuta hayo kwenye sehemu za ndani ya mwili, kuuzunguka moyo, na ndipo matatizo yanapoanza.
Utapimaje Tumbo Lako?
Kuna njia za kitaalamu za kupima kiasi cha mafuta ya ndani uliyo nayo ambazo ni CT Scan au MRI lakini pia unaweza kujipima mwenyewe ukapata picha nzuri tu ya hali yako. Chukua kipimo cha utepe, kile kinachotumiwa na mafundi cherehani (measuring tape), jipime eneo la kitovuni ukiwa umesimama huku ukihakikisha kuwa utepe ni mnyoofu. Kwa afya nzuri, kipimo kisizidi nchi 35 kwa mwanamke na kisidi nchi 40 kwa mwanamme.
Kuwa na mwili wenye umbo la pears “pear shape”, hips na mapaja makubwa, kunafikiriwa kuwa ni bora zaidi ya umbo la apple ambalo linamaanisha kiuno kipana zaidi. Kuwa na kiuno kipana kuna uwiano na kiasi cha mafuta ya ndani (visceral fat) uliyo nayo.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data