CHANZO NA TIBA: UVIMBE KWENYE KIZAZI

CHANZO NA TIBA: UVIMBE KWENYE KIZAZI - Tanzania
  • CHANZO NA TIBA: UVIMBE KWENYE KIZAZI - Tanzania
Description :

Fahamu kuhusu Uvimbe kwenye kizazi na namna ya kujitibu

Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama ‘uterine myoma’ au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.

Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke.

Ni uvimbe ambao hauhusiani na kansa na unaweza kubadilika rangi ukawa wa njano, unaweza kubadilika ukawa kama maji tu na kurudi tena kuwa mgumu.

Uvimbe kwenye kizazi hujulikana pia kwa majina haya kitaalamu: ‘Uterine fibroids’, ‘Myoma’ au ‘fibromyoma’.

Hujulikana pia kama ‘leiomyoma’ katika lugha ya kidaktari. Wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 50 ndiyo wanapatwa kirahisi zaidi na ugonjwa huu.

CHANZO cha moja kwa moja cha ugonjwa huu bado hakijulikani wazi, hata hivyo baadhi ya sababu za kutokea huu uvimbe ni pamoja na;

1. Kuongezeka sana vichocheo vya progesterone na estrogen kuzidi kiwango mwilini.
2. Ujauzito.
3. Uzito na unene kupita kiasi.
4. Jenetiki zisizo za kawaida.
5. Mfumo usio sawa wa mishipa ya damu.
6. Sababu za kurithi.
7. Lishe isiyo sawa.
8. Sumu na taka mbalimbali n.k.

DALILI zitakazokuonyesha una uvimbe kwenye kizazi ni pamoja na;

1. Kupata damu nyingi wakati wa hedhi.
2. Maumivu makala wakati wa siku za hedhi.
3. Kuvimba miguu.
4. Unaweza kuhisi una ujauzito.
5. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
6. Kuhisi kuvimbiwa.
7. Kupata haja ndogo kwa taabu.
8. Kutokwa na uchafu ukeni.
9. Kupata choo kigumu au kufunga choo.
10. Maumivu nyuma ya mgongo.
11. Maumivu katika miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuwaka moto.
12. Upungufu wa damu.
13. Maumivu ya kichwa.
14. Uzazi wa shida.
15. Kutopata ujauzito.
16. Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo.
17. Maumivu ya nyonga.
18. Mimba kutoka mara kwa mara (miscarriage).

AINA ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI

Kuna aina kuu nne za Fibroids

1. Intramural: Hutokea kwenye kuta za mji wa mimba (uterus). Wanawake wengi hupatwa na aina hii ya uvimbe.

2. Subserosal fibroids: Hii hukua nje ya kuta za mji wa mimba na hukua na kuwa kubwa sana.

3. Submucosal fibroids: Hutokea kwenye misuli chini ya ngozi laini ya kuta za mji wa uzazi.

4. Cervical fibroids: Hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix).

TIBA
Mara nyingi hospitali wamekuwa wakifanya
Upasuaji kuondoa Uvimbe ingawa kumekuwa na changamoto ya kuharib kabisa kizazi.

USHAURI
Kama umesha pima ukagundua una Uvimbe. Wasiliana nasi kupata TIBA LISHE kuondoa Changamoto kabisa ya UVIMBE bila madhara wala Chemikali

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data