jinsi Ya Kutibu Vidonda Tumbo Kwa Urahisi

 jinsi Ya Kutibu Vidonda Tumbo Kwa Urahisi - Tanzania
  •  jinsi Ya Kutibu Vidonda Tumbo Kwa Urahisi - Tanzania
Description :

Fahamukuwa Katika afya binadamu mfumo wa njia ya chakula ukiusisha tumbo ni muhimu sana katika kuhakikisha kila mtu anapata afya sahihi na kitu ambacho ulikuwa ukijui ni kwamba Zaidi ya asilimia 75% magonjwa yote huanzia tumboni,na hii ni kwasababu afya zetu huimarishwa na vyakula tulavyo hivyo kama mfumo mzima wa njia ya chakula hauko vizuri basi inakuwa hatari kubwa sana ya kudhoofisha mwili na afya kwa ujumla.Baada ya kufahamu hayo ni muhimu sasa sisi sote tuelewe nini tunamaanisha hasa tunapozungumzia vidonda vya tumbo hasa jinsi vinavyoweza kutokea,dalili zake na madhara kwa ujumla ili uweze kudhibiti tatizo hili kukupata na kuliondoa kama uko nalo tayari.Tuanze na maana harisi kwanza nini maana ya vidonda vya tumbo.
NINI MAANA YA VIDONDA VYA TUMBO NA HUSABABISHWAJE
Vidonda vya tumbo hii ni ile hali yakuwa na vidonda au michubuko kwenye ukuta (membrane) mwembamba na laini sana watumbo lako la chakula.Naviko vitu kadhaa ambavyo huweza kusababisha changamoto hii ya vidonda katika tumbo lako la chakula,sasa vifwatavyo ni mambo au sababu zinazopelekea mtu kupata vidonda vya tumbo;
· Helicobacter pylori;huyu ni bacteria ambae ndie anaeleta maambukizi haya ya vidonda vya tumbo inasemekana kuwa bacteria huyu tunaishi nae tumboni kwa kipindi kirefu tu lakini mwisho wasiku huperekea madhara makubwa sana katika kuathiri ukuta wat umbo lako la chakula na hatimaye kupata vidonda vya tumbo.

· Matumizi ya madawa ya kuondoa maumivu; tumekuwa tukiishi na kuyapa sana kipaombele hasa haya madawa ya kikemikali sasa kitu ambacho unapaswa kukifahamu sasa ni kwamba huu utumiaji wa madawa ya kupunguza maumivu kama Panadol,ibuprofen,pamoaja na asprine kwa Zaidi ya asilimia 50% huchangia kupata vidonda vya tumbo,na imekuwa mazowea sasa kichwa kikiuma kidogo unatafuta dawa ya maumivu bila kujua unazidi kuhatarisha afya yako.
· Mtindo halisi wa kimaisha;hapa tunazungumzia sasa maisha ambayo umeyachagua kuyaishi kwa namna moja au nyingine huweza kuchangia kupata vidonda vya tumbo kama utumiaji wa madawa mfululizo,msongo mawazo na hasira kila wakati,kutumia vyakula vyenye acid nyingi wakati tumbo liko empty au halina kitu kama machungwa,kahawa,lakini pia huvutaji sigara nao unachangia pia wewe kupata vidonda vya tumbo.Hizo ndizo sababu au makundi matatu makubwa humfanya mtu aweze kupata vidonda vya tumbo ingawa ziko asilimia chache sana watu hupata vidonda vyatumbo yabila sababu kufahamika lakini pia kwa asilimia chache watu hupata vidonda vya tumbo kwasababu ya kurithi.Sasa ni muhimu hapa kuwa makini na afya yako ili kuakikisha unadhibiti ipasavyo tatizo hili, kama nilivyosema mwanzo wengi huwa ningumu kufahamu kama wako na hili tatizo kwa pamoja sasa hebu tuone nini hasa dalili za vidonda vya tumbo ili ukiwa nazo basi uchukue hatua kwa haraka;
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Ukiona unadalili hizi tajwa hapo chini moja au Zaidi kwa muda kadhaa na ukuwai kufikilia wala kuwaza kama labda kuna uhusiano na vidonda vya tumbo basi ni vyema ukachukuwa hatuwa mapema;
-Maumivu makali ya tumbo upande wa juu hii ni hali ambayo inawakuta watu wengi sana na mara nyingi maumivu haya yaweza kuwa kuisi kama tumboni kunawaka moto na kuungua sana au yakawa ya kuchoma Zaidi basi juwa wazi kuwa hizo ni dalili za mwanzo za vidonda vya tumbo.
-Kiungulia hii ni ile hali yakupata kiungulia na tumbo huwa lina jaa gas sana kiasi kwamba hupelekea mtu kushindwa kujiskia vizuri kwa tumbo lake na mfumo mzima wa njia ya chakula,sasa kitu kinachopelekea wewe upate kiungulia ni kwasababu tu ya kiwango cha acid kinachozalishwa mwilini mwako ni kingi na hakitumiki ipasavyo hivo ile acid inaunguza sehemu zile zenye vidonda au michubuko katika ukuta wat umbo lako la chakula.
-Kupata kichefufu,kutapika,na kuharisha hapa tunazungumzia kupata mchafuko wa njia hii ya chakula moja kwa moja naivo kupelekea kupata kichefuchefu na kukosa hamu ya kula kabisa kwasababu ya kutapika na kwenda chooni kwajili ya haja kubwa ambayo kiasi kwamba inakumaliza mpaka nguvu za mwili.

Our safety tips

  • Listings with a "Shop" tag means that the publisher was curated by Jumia.
  • At all costs, avoid paying before seeing the item.
  • Avoid sending money through untraceable methods such as Western Union or Mobile Money.
  • Thoroughly check the item to make sure it's matches the assumed condition.
  • If the seller doesn't have a shop, meet with him in a public place (Mall, Gas station, workplace ...).
  • Do not give personal details (bank details, credit card numbers ...).
  • Beware of offers that are too good to be true.

What do you have to sell?

Sell everything for free on jumia.co.tz!

Post a Free Ad Now!
Processing data